MBUNGE wa
jimbo la Mkuranga Mkoani Pwani na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah
Ulega ametembelea katika Kitongoji cha Churwi, Kata ya Tambani na kukaguwa mradi wa kivuko
ambapo amefanikiwa kutatua changamoto ya
kivuko hicho chenye historia ya kuuwa watoto wawili.
Akizungumza
na wananchi wa eneo hilo, Ulega alisema kuwa ameridhishwa na kitendo cha
wananchi kuweza kujichangisha na kuanza ujenzi wa kivuko ili kukabiliana na
changamoto zilizokuwa zikiwakabili za kukosa kivuko kwa muda wa miaka mingi.
Katika hali
hiyo imempelekea Naibu waziri huyo kuchangia
mifuko ya saruji 60 na milioni moja na
nusu kuongeza nguvu katika ujenzi wa
kivuko hicho.
Aidha amewataka wananchi hao kuongeza ushirikiano zaidi katika
masuala ya maendeleo kwani wananchi
wanapoanzisha miradi ya maendeleo serikali
ni lazima iweke mkono wake ili
kuongeza nguvu.
"Tushirikiane
ili kuokoa maisha ya watoto wetu pia
kivuko hiki kitasaidia kufungua
fursa mbalimbali za maendeleo kutokana
na uwepo wa uhakika wa njia"Alisema
Ulega.Kwa upande wake diwani wa kata
hiyo Ally Mtamirwa amempongeza mbunge
Ulega kwa juhudi zake anazozifanya katika kuhakikisha mkuranga ina kuwa
ya kuigwa kwenye maendeleo.
Aliongeza kuwa bado
wananchi wanaendelea kujitolea katika mambo mbalimbali ya maendeleo ili
kuhakikisha wanafanikiwa katika upatikanaji wa huduma za jamii.
Mbunge wa jimbo la Mkuranga mkoa Pwani, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah
Ulega akimkabidhi diwani wa kata ya
Tambani, Ally Mtamiwa mifuko 80 ya saruji kwaajili ya ujenzi wa kivuko katika
kitongoji cha Churwi kata ya Tambani
wilaya ya Mkuranga.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
Mbunge wa jimbo la Mkuranga mkoa Pwani,Naibu Waziri
wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiweka jiwe la msingi ujenzi zahati ya
kijiji cha Tipo ambapo alichingia amifuko 50 ya saruji na shilingi milioni
moja.
Mbunge wa jimbo la Mkuranga mkoa Pwani, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah
Ulega akiwa ameongoza na niongozi wa chama cha (CCM) wa wilaya hiyo wakigangua
mradi wa Zahanati ya kijiji cha Tipo ambapo alichangia mifuko 50 ya saruji na shilingi milioni moja.
Muuguzi wa
hospitali ya wilaya ya Mkuranga ,Grace Msemwa akisisitiza jambo katika mkutano
uliofanyika katika kijiji cha Tipo wilaya ya hiyo.
Muonekano wa
kivuko kinachoendelea kujengwa katika kitongoji cha Churwi kata ya Tambani wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...