Mwanamuziki Ahmed Kipande, alishiriki kikamilifu katika uhamasishaji wa maendeleo na kupigani Uhuru wa Tanganyika akiwa na bendi yake ya Kilwa Jazz.

Bendi hiyo ilishiriki kikamilifu siku Tanganyika inapata Uhuru Decemba 09, 1961 kwa kimba wimbo wa kusifia nchi yetu kupata Uhuru toka wa Wakoloni wa Waingereza.

Aidha chini ya uongozi wake Ahmedi Kipande, bendi yao ilishiriki kikamilifu kutoa burudani wakati mikakati ya kufanya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye meneo ya Makao Makuu ya bendi hiyo jijini Dar es Salaam mwaka 1964.

Juhudi zao katika muziki zilipelekea kuteuliwa na serikali ya Tanganyika kwenda kushiriki sherehe za Uhuru wa nchi za Malawi na Uganda.

Wasifu wa Ahmed Kipande iliyoelezewa na mwanawe wa mwisho Kipande Ahmed, alesema kwamba jina kamili la  baba yake alikuwa ikiitwa Ahmed Mohammed Kipande.Mrisho alitamka kuwa baba yake alizaliwa mwaka 1937, huko Kilwa Kivinje mkoani Lindi.

Miaka michache baada ya kifo cha mama yake Ahmed Kipande alifuatana na baba yake kuja Dar es Salaam. Baada ya kufika,  na alianza masomo katika shule ya Uhuru Wavulana maeneo ya Kariakoo, jijini Dar es Salaam.

Katikati ya miaka ya 1950, Kipande alianza kupiga muziki akitumia ala iitwayo Violin, katika bendi ya Tanganyika Jazz iliyokuwa ikiongozwa na Zimbe Kidosi.Bendi hiyo ilikuwa  na makao makuu yake mtaa wa New Street ambao hivi sasa unaitwa Lumumba.

Wanamuziki wa miaka hiyo walianzisha bendi wakizipa majina ya maeneo yale  wanakotoka. Hivyo waanzilishi wa Rufiji Jazz walitoka Rufiji, na ndivyo ilivyokuwa kwa Kilwa Jazz, Ulanga jazz na kadhalika.
Ahmed Kipande aliyekuwa ametoka Kilwa Kivinje mkoani Lindi, nae akishirikiana na mwanamuziki mwenzake aliyetajwa kwa jina moja la Shamte, wakaamua kuanzisha bendi ya watu kutoka Kusini ya Kilwa Jazz mwaka 1958.

Kilwa Jazz ikaanza kujizolea umaarufu kwa kutunga na kuimba nyimbo mbali mbali zikiwemo za siasa, mapenzi na za uhamasishaji kupata Uhuru wa Tanganyika.Kipande alitunga na kuimba wimbo wa TANU yajenga nchi, nchi yetu,  enyi Vijana tujenga yetu Doli na It can be done, play your party.

Zingine zilikuwa za Roza waua,‘Nipate lau nafasi, Nacheka cheka Kilwa leo na ule wa  Maneno hayafai

Nyimbo hizo zote zilizotajwa hapo juu, Ahmed Kipande na wanamuziki wa bendi hiyo walifanya kukopi nyimbo toka Jamhuri wa Kidemokrasia ya Kongo akina Tabu Ley na John Bokelo.Wimbo wa ‘Mokolo Nakokufa’ halikadhalika nyimbo za Nacheka cheka Kilwa leo na Maneno hayafai ambazo kwa ujasiri wao ‘waliukopi na kupesti’ toka wimbo wa Course au Povouir wa T.P.OK. Jazz.

Mwaka 1973 Kilwa jazz ilialikwa na kutumbuiza kabla ya onyesho la gwiji la muziki wa dansi, Franco Luambo Makiandi na bendi ya T.P.OK. Jazz  iliyefanya onyesho kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Luambo Makiadi baada ya kuzisikiliza nyimbo hizo, alimfuata Ahmed Kipande na kumpongeza kwa umahiri wake mkubwa wa ‘kokopi na kupesti’ pasipo kukosea.

Mrisho akimsifia baba yake Kipande Ahmed, alisema kwamba mwaka 1961 siku Tanganyika inapewa Uhuru toka kwa Wakoloni, bendi ya Kilwa Jazz ilikuwa Uwanja wa taifa ikiporomosha muziki ambapo ilitoka na wimbo wa  kumshukuru mungu kwa kupata Uhuru.
Mtoto huyo japom hakuwepo wakati huo, ameukariri wimbo huo wa marehemu Ahmed. Aliimba mistari michache ya wimbo huo.
 “ Ewe mola tunakuomba uibariki Tanganyika yetu na jirani  zetu, Uhuru tumepata lakini Nyoyo zina sikitika wenzetu wanateseka  Wakoloni wa mewashika…”
Bendi ya Kilwa Jazz ilikuwa na makao makuu yake katika kona ya mitaa ya Muhoro na Jangwani ambako siku moja ilipiga muziki nje ya ofisi yao, iliwashangaza watu kuona bendi hiyo ikipiga muziki mchana.
Lakini ilikuwa mipango kamambe ikipangwa maeneo hayo kwa viongozi Wanamapinduzi siku chache kabla ya mapinduzi ya Zanzibar viongozi wakipanga mikakati ya mapinduzi yaliyouondoa utawala wa Kisultani mwaka 1964 huko Zanzibar.
Bendi ya Kilwa Jazz baadaye haikuelewa na jamii. Wengine wakafika mbali zaidi wakizusha maneno kwamba bendi hiyo ni ya serikali. Sababu eti ilikuwa ikialikwa kutoa burudani katika sherehe nyingi za kitaifa!
Bendi hiyo pia ilialikwa kutoa burudani katika sherehe za ndoa ya mmoja wa mawaziri wa serikali ya Tanganyika wakati huo, Oscar Kambona.

Ahmed  Kipande katika sherehe hiyo alionesha kipaji chake kwamba si cha kubahatisha.
Alitunga wimbo wa papo kwa papo wa kuwasifia wanandoa hao Oscar Kambona na mkewe.

Yaelezwa kwamba Kambona aliinuka toka kwenye kiti cha maharusi na  kwenda kumkumbatika Kipande kisha akamtuza kwa pesa. 
Ni miaka 32 sasa tangu Ahmedi Mohammed Kipande afariki dunia  Aprili 27, 1987 baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi kwa kipindi kirefu.
Kipande alizikwa kwenye  makaburi ya Tandika Maguruwe, mkoani Dar es Salaam  Aprili 28,1987.

Mugu ailaze roho ya marehemu Ahmedi  Kipande  pahala pema peponi, amina.  

Mwisho.
Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa  namba: 0713331200, 0767331200, 0736331200 na 0767331200

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...