Vijana wa kikundi cha Nyati katika Kijiji cha Mwabulutago Kata ya Mwasengela wakikabidhiwa mashine ya kuchomelea itakayochangia uchumi wa jamii yao.
Wanakikundi cha uzalishaji mali Kijiji cha Makao wakikabidhiwa moja na Mkuu wa wilaya ya Meatu,Dk Joseph Chilongani.
Wanawake walionufaika kwa kujengewa uwezo wa kuweka na kukopa wakimpa zawadi Meneja wa Maendeleo ya Jamii wa kampuni ya FCFL,Nana Woodley.
Mkuu wa wilaya ya Meatu mkoa wa Simiyu,Dk Joseph Chilongani akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa mbalimbali kwa wananchi wake,kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Meatu,Juma Mwiburi na Meneja wa FCFL,Nana Woodley.
Mkuu wa wilaya ya Meatu mkoa wa Simiyu,Dk Joseph Chilongani(wa pili kushoto) akimsikiliza mkulima wa Kijiji cha Matale Kata ya Tindabuligi,Sayi Luchagula alipotembelea shamba lake lililowekewa uzio wa mizinga ya nyuki ili kuwazuia Tembo kushambulia mazao yao.
Mkuu wa wilaya ya Meatu mkoa wa Simiyu,Dk Joseph Chilongani(wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya Friedkin Conservation Fund Limited pamoja na viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Meatu.


Vijiji Sita vinavyozunguka Pori la Akiba la Maswa na Hifadhi ya Jamii ya Wanyamapori ya Makao wilaya ya Meatu mkoa wa Simiyu vimenufaika kwa kuwezeshwa elimu ya kuweka na kukopa pamoja na ufugaji wa nyuki kwaajili ya kujikwamua kiuchumi.

Mkuu wa wilaya ya Meatu mkoa wa Simiyu,Dk Joseph Chilongani akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa vya kuwawezesha wananchi kiuchumi viliyotolewa na kampuni ya Utalii ya Friedkin Conservation Fund(FCF) vyenye thamani ya Sh 55 milioni aliwataka wananchi kuvitumia kujiletea maendeleo.

Alisema utaratibu uliofanywa na kampuni hiyo kuwapa elimu ya ujasirimali na kutoa nyenzo mbalimbali za kufanyia kazi zikiwemo mizinga ya nyuki,mashine za kuchomelea na vifaa vya kusindika asali utasaidia kuwapa wananchi fursa za kutumia mazingira yanayowazunguka kujiongezea kipato.

“Napenda kuwashukuru wadau wetu wa maendeleo kwa mchango mnaoutoa katika kusaidia jamii hii najua sio mara ya kwanza na mtaendelea kufanya hivyo kwasababu wananchi wetu wanaohutaji wa aina mbalimbali lakini wanashindwa namna ya kuanza ,”alisema Chilongani

Vijana Magese Donald na Koyo Ndimila kikundi cha Nyati katika kijiji cha Mwamhongo Kata ya Mwasengela waliopewa mashine ya kuchomelea yenye thamani ya Sh 6 milioni walisema itawasaidia kuongeza kipato na kupunguza ukataji miti kwaajili ya kutengeneza vifaa mbalimbali.

Ndimila alisema ujuzi walionao wa kutengeneza madirisha,milango na vitanda vya chuma utapunguza ukataji wa misitu ambao unaathiri vyanzo vya maji na mazingira kwa ujumla hivyo utatoa fursa kwao kujikwamua kiuchumi.

Afisa Maendeleo ya Jamii ya kampuni ya FCF,Alfred Mwakivike alisema vijiji zaidi ya 20 vinavyopakana na Pori la Akiba la Maswa pamoja na Hifadhi ya Jamii ya Makao mashamba ya wakulima yamekua yakivamiwa na wanyamapori wakubwa na kuwasababishia hasara.

Alisema wametoa mizinga 53 ya nyuki na kuweka uzio kwa mkulima Sailu Chagula kwenye shamba lake hatua iliyozuia wanyamapori wakubwa hasa Tembo kuacha kuvamia shamba hilo na mashamba yaliyo jirani.

“Tunapenda wakulima waendelee na shughuli zao na kupata tija bila kuwaona wanyamapori kama kikwazo kwao kwasababu wanao mchango muhimu katika kukuza pato la taifa,tumewapa mbinu ya kutumia mizinga ya nyuki kuwazuia Tembo kuvamia mashamba yao na wameipokea vizuri,”alisema Mwakivike

Vijiji vilivyonufaika na miradi ya maendeleo ni Matale,Sapa,Makao, Mwamhongo ,Mwabutulago na Mbushi ambavyo vimenufaika kwa kupewa mizinga ya nyuki,miradi ya elimu,Ujasiriamali na miradi ya maji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...