*Ili kufanikiwa ni lazima nidhamu ipewe kipaumbele
 *Muamuzi afungiwa Msimu mzima kutokana na utovu wa nidhamu
     
       Na.Khadija seif,Globu ya jamii

CHAMA cha soka visiwani Zanzibar (ZFA) kupitia kamati ya kusimamia mashindano ya soka na ligi ya Zanzibar kitaifa, imemfungia kwa mwaka mmoja, mwamuzi, Ramadhan Keis, kutokana na makosa mbalimbali ya utovu wa nidhamu.

Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Hussein Ahmada, ameeleza kuwa kama kamati ilijaribu mara kadhaa kumuonya mwamuzi huyo, lakini, alionekana kutokuwa na nia ya kubadilika katika uchezeshaji wake pamoja na kutokuwa na nidhamu kwa wakuu wake wa kazi.

“Tumemuonya mara kadhaa, lakini, hakuonyesha kubadilika, tumeona bora tumsimamishe”, alisema Ahmada.Aidha ahmada amesema katika tukio la hivi karibu, mwamuzi huyo alikataa kuchezesha mechi kati ya Negro na Zantex kwa madai kuwa kamishna aliyepangiwa hakukubaliani nae.

Na pia kitendo hicho kilikuwa cha utovu wa nidhamu jambo ambalo kama kamati imeona bora wamfungie na kumuangalia kwa msimu ujao kama atabadilika waweze kumsamehe.

“kimsingi muamuzi huyo hayuko tayari kubadilika, hivyo tumemfungia msimu mzima na mbali na hayo pia huwa ni mgumu wa kuandika hata ripoti wakati anapomaliza kuchezesha mechi zake”, alisema Ahmada.

Na ameitaka  kamati iliyopo kwa sasa kuwa na nidhamu michezoni na kuheshimu viongozi wa kila nyanja hususani kwa viongozi wa juu ,ili kufanikiwa ni lazima kuipa kipaumbele nidhamu kwa watu wote wanaokuzunguka ndipo utafanikiwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...