Na. Vero Ignatus, Arusha

Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa jangwa la Sahara( MISA) imeendesha mjadala wa siku moja wawaandishi wa habari, na wadau mbalimbali vya habari Jijini Arusha katika chuo cha Uandishi wa habari cha Fanikiwa ikiwa na lengo la kujadili changamoto zilizopo kwenye vyombo vya habari.

Gasirigwa Sengiyumva ni Mkurugenzi wa MISA nchini amesema kuwa lengo kuu la mjadala huo ni kuboresha namna ambayo vyombo vya habari vinafanya kazi, kukuza uhuru wa habari, kupata habari, uhuru wa vyombo vya habari

Amesema kuwa upo umuhimu wa waandishi wa habari kuzingatia maadili ya uandishi, kuendana na sheria ya habari ya mwaka 2016 na kumtaka kila mwandishi kutimiza wajibu wake kwa kutafuta ukweli wa habari na uripoti ukweli sahihi, na kuepuka kuandika habari zinazodanganya jamii

Kwa upande wake mjumbe wa bodi ya MISA nchini Tanzania Mussa Juma amesema kuwa ni vyema waandishi wa habari kuepuka uchochezi unaokinzana na maslahi ya Taifa kwani kulingana na sheria ya habari ya mwaka 2016 kosa la mwandishi ni faini ya shilingi milioni 3,na kifungo hadi miaka 3

Pia amesisitiza waandishi kujiongeza Kielimu kwani serikali ilitoa kipindi cha miaka mitano kuanzia januari 01,2017 ndipo ilipitiswa kuwa kila mwandishi wa habari kuwaanzia kiwango cha diploma ya uandishi wa habari kutoka vyuo vinavyotambulika.

Wakichangia mjadala huo, Mwenyekiti wa Arusha Press Klabu, Claud Gwandu kushirikiana na wadau kudai mabadiliko ya sheria ya huduma za habari amesema kuwa sheria hiyo ina mapungufu kadhaa, ikiwepo kutotambua kada za chini katika vyombo vya habari, ambazo hazihitaji kuwa na elimu ya diploma na pia kufanya makosa ya habari kuwa makosa ya jinai.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha uandishi wa habari cha Fanikiwa Bwana Andrea Ngobole amesema kuwa siyo kweli kwamba hawatoi elimu ya kutoshawaandishi watarajiwa katika vyuo vyao bali wanatoa sawasawa na mtaala toka Nacte ila wanapokwenda nje ya chuo wanakutana na shinikizo la muda na kiuchumi wa habari tofauti ambazo kile jamii inahitaji kusikia.

Amekubaliana hoja wadau wa mkutano huo wa kuwachukua wataalamu wa habari wenye uzoefu wa muda mrefu ili waweze kutoa mafunzo yenye uhalisia katika tasnia ya habari ili waweze kutoa taarifa zenye uhalisia wa maisha ya watu wengi.

Kwa upande wake Inspekta wa polisi Rashid Nchimbi ambae amemuwakilisha RPC Jonathan Shana amesema jeshi polisi wanaushirikiano na waandishi hivyo yapo madawati mengi ambayo wanaweza kupata habari za kipolisi kila leo wakihitaji wasikariri sehemu moja.

Pia amewashauri vyuo vya uandishi wa habari kutafuta waalimu wenye uzoefu na kazi hiyo kwaajili ya kutoa mafunzo kwani asilimia kubwa wanakauwa na uzoefu mkubwa na kazi wanayoifanya.Nae Mkurugenzi Civic and Legal Aid Organization (CiLAO)amesema kuwa wanajiandaa kufanya mkutano na wadau wa Habari, haki za binadamu, tume ya uchaguzi nchini na Tamisemi ili kuona namna Waandishi wa Habari watashiriki kwenye uchaguzi kama waangalizi wa uchaguzi.

''Tayari tumefanya utafiti kwenye uchaguzi mkuu nchini Kenya ambako Vyombo vya Habari vina haki ya kushiriki katika mchakato mzima wa uchaguzi kuanzia upigaji, uhesabuji wakiwa ndani kama ambavyo waangalizi wa uchaguzi walivyo na haki hiyo"alisema Odero Odero

Gasirigwa Sengiyumva ni Mkurugenzi wa MISA nchini akizungumza na waandishi wa habari na wadau wa habari
Baadhi ya washiriki wa mjadala wa changamoto za vyombo vya habari na namna vinavyofanya kazi
Baadhi ya washiriki wa mjadala wa changamoto za vyombo vya habari na namna vinavyofanya kazi
Mjumbe wa bodi ya MISA nchini Tanzania Mussa Juma akifafanua juu ua sheria mpya ya habari ya mwaka 2016
Mkuu wa Chuo cha uandishi wa habari cha Fanikiwa Bwana Andrea Ngobole akuchangia mjadala kuhusiana na elimu kwa wanaandishi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...