Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula akizungumza na wanawake wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanyika machi 8 mwaka huu katika ukumbi wa taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi wa JKCI Dkt. Delila Kimambo
Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Agnes Kuhenga akielezea namna ambavyo wanawake wa taasisi hiyo walivyoanzisha kampeni ya kuwasaidia wanawake na watoto katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani wakati wa hafla fupi ya kuhitimisha siku ya wanawake duniani iliyofanyika machi 8 mwaka huu katika ukumbi wa taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya viongozi wanawake kutoka katika taasisi za afya wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokua yakiendelea wakati wa hafla fupi ya kuhitimisha siku ya wanawake duniani iliyofanywa na wanawake wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) machi 8 mwaka huu katika ukumbi wa taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula akimkabidhi baba wa mtoto mwenye magonjwa ya moyo Richard Zaya kiasi cha shilingi 593,000 kilichotolewa na umoja wa wanawake wa JKCI kusaidia matibabu ya mtoto huyo wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanywa na wanawake wa JKCI machi 8 mwaka huu katika ukumbi wa Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam
Baadhi wa wanawake wa Taasisi ya moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanywa na wanawake hao machi 8 mwaka huu katika ukumbi wa taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi na Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Delila Kimambo akimshukuru mgeni ramsi kushirikiana na wanawake wa JKCI kuadhimisha siku ya wanawake duniani wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha siku hiyo iliyofanyika machi 8 mwaka huu katika ukumbi wa taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula akicheza mziki na wafanyakazi wanawake wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanywa na wanawake wa JKCI machi 8 mwaka huu katika ukumbi wa taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam

Baadhi ya wanawake wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) katika picha ya pamoja wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanywa na wanawake hao machi 8 mwaka huu katika ukumbi wa taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam

…………………………..

Na Anna Nkinda

Wafanyakazi wanawake wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wametakiwa kushirikiana na kutengenezeana fursa mbalimbali za maendeleo ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Idara Kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula wakati akiongea na wafanyakazi wanawake wa Taasisi hiyo katika sherehe ya kuadhimisha siku ya mwanamke Duniani.

Dkt. Chaula alisema ni muhimu kwa kila mwanamke akahakikisha anatengeneza fursa ya mafanikio kwa mwenzake jambo la muhimu ni kupendana, kushikana mkono na kuhakikisha hakuna mtu atakayefukuzwa kazi na atakayetamani kustaafu kabla ya wakati.

“Hakikisheni mazingira ya kazi yanakuwa mazuri na salama kwenu ninyi wote, kushirikiana kwenu kutawawezesha kufika mbali zaidi katika utendaji wenu wa kazi kwani katika mafanikio yoyote yale mchango wa mwanamke ni mkubwa zaidi ukilinganisha na wa mwanaume”, alisema Dkt. Chaula.

Aliendelea kusema kuwa katika sehemu ya kazi kila mtu anamchango katika mafanikio ya mwenzake, ukiona umefanikiwa tambua nyuma yako kuna watu wamekufanya ukafika hapo ulipo hivyo basi ni muhimu kwa wafanyakazi hao kuwa karibu zaidi.

Dkt. Chaula alimalizia kwa kuwataka wanawake hao kumtanguliza Mungu katika kazi zao za kila siku kwani kwa kufanya hivyo watakuwa na familia njema zenye hofu ya Mungu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tiba Shirikishi Dkt. Delila Kimambo alisema katika kuadhimisha siku ya wanawake Duniani wafanyakazi wanawake wa Taasisi hiyo walifanya upimaji wa viashiria vya magonjwa ya moyo pamoja na kutoa elimu kwa wanawake wa soko kuu la Kimataifa la Samaki la Feri pamoja na maeneo jirani.

Dkt. Delila ambaye ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo alisema waliamua kwenda kupima magonjwa ya moyo na kutoa elimu kwa wanawake wa Soko hilo kwa kuwa hawana muda wa kwenda kupima afya zao.

“Tuliwafundisha viashiria vya hatari vya magonjwa ya moyo kwa wanawake na kuwapima afya zao. Tafiti zinaonyesha kuwa ukitoa elimu ya magonjwa ya moyo kwa wanawake kwa asilimia 80 utapunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo katika jamii”, alisema Dkt. Delila.

Katika kuadhimisha siku hiyo wafanyakazi hao walichanga kiasi cha shilingi 593,000/= fedha ambazo walimkabidhi baba mzazi wa mtoto Yasinta Zaya (15) ambaye amelazwa katika Taasisi hiyo kwa ajili ya matibabu ya moyo.

Akizungumza kabla ya kuzikabidhi fedha hizo Daktari bingwa wa usingizi na wagonjwa walioko katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) Anjela Muhozya alisema waliamua kumsaidia mtoto huyo ambaye alianza kuumwa ugonjwa wa moyo akiwa na umri wa miaka sita.

“Mtoto huyu anasubiri kwenda kupatiwa matibabu nchini Israel, hivi sasa afya yake imebadilika amelazwa ICU anatakiwa kufanyiwa vipimo mbalimbali ikiwemo MRI (Magnetic Resonance Imaging – MRI. Tumeona tumsaidie kwani wazazi wake hawana uwezo”, alisema Dkt. Anjela.

Akiongea mara baada ya kupokea fedha hizo Baba mzazi wa mtoto huyo Richard Zaya ambaye ni mkazi wa Kalambo mkoani Rukwa aliwashukuru wafanyakazi hao kwa moyo wa upendo waliouonyesha kwa mtoto wake na kuomba waendee kufanya hivyo kwa watu wengine wenye uhitaji.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Dkt. Chaula alitoa kiasi cha shilingi milioni moja na elfu hamsini kati ya hizo shilingi milioni moja itatumika kwa ajili ya vipimo vya mtoto huyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...