Na Sultani Kipingo
Wapenzi wawili mjini Cape Town, Afrika ya
Kusini, wamefunga ndoa hospitalini siku moja baada ya bwana harusi kushambuliwa
na majambazi nyumbani kwake .
Muneer Hercules na Maryam Kallie walifunga
pingu za maisha katika hospitali ya Melomed Gatesville Jumapili Machi 10, 2019,
huku bwana harusi akiwa kitandani na Bi harusi pembeni yake.
Kwa mujibu wa ukurasa wa Facebook wa Melomed
Gatesville, Hercules alikimbizwa hospitalini hapo baada ya kujeruhiwa na
majambazi nyumbani kwake Jumamosi Machi 9.
"Asubuhi hii Muneer Hercules na Maryam
Kallies wamefanya Nikkah mbele ya watu wa familia zao hapa Melomed Gatesville Hospital. Muneer alishambuliwa
usiku wa kuammia leo na kukimbizwa hospitali.” Ameandika Melomed.
Hata hivyo, shambulizi hilo halikuzuia wapenzi
hao kuoana kwa taratibu za Kiislamu hapo hospitali, na mapicha kibao yaliyo
kwenye ukurasa wa Melomed yanaweza kukufanya utokwe na chozi.
Maryam alikuwa amevaa shela lake nzuri nyeupe
huku mkononi kashikilia maua wakati akiingia hospitalini hapo, wakati mumewe
mtarajiwa akiwa anasubiri kwa hamu kitandani huku akipigana na maumivu, bila
shaka akimshukuru Mola kwa kumjaalia mwenza atayeishi naye kwa shida na raha.
Muneer Hercules na Maryam Kallie wakikumbatiana baada ya kufunga za maisha katika hospitali ya Melomed Gatesville Jumapili Machi 10, 2019,
Muneer Hercules na Maryam Kallie walifunga pingu za maisha katika hospitali ya Melomed Gatesville Jumapili Machi 10, 2019,
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...