WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakandarasi wanaojenga majengo mbalimbali nchini yakiwemo na ya Serikali wahakikishe wanazingatia viwango na waache kulipua kazi.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amewataka wakandarasi wawafundishe kazi mafundi wasaidizi wanaowatumia katika ujenzi wa miradi malimbali ili waweze kunufaika kwa kuongeza ujuzi.

Ametoa wito huo  leo mchana (Jumamosi, Machi 16, 2019), alipotembelea miradi mbalimbali ya ujenzi wilayani Ruangwa mkoani Lindi, ukiwemo wa Hospitali ya wilaya.

Amesema Serikali inatoa pesa kulingana na kazi inayotakiwa kufanyika, hivyo amewataka wakandarasi wafanyekazi wanazopewa kwa kufauata taratibu za kiufundi na si ‘kulipua lipua’.

Pia, Waziri Mkuu amewaagiza wakandarasi hao kuwatumia mafundi wasaidizi waliopo kwenye maeneo ya karibu na miradi husika ili nao waweze kupata ajira.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amewataka mafundi wasaidizi wahakikishe wanafanyakazi kwa bidii na uadilifu ili wawe mabalozi wazuri, jambo litalalowawezesha wengine kupata kazi.

"Nataka niwaambie mkifanya kazi kwa uaminifu wakandarasi.

watawachukua na kuwapeleka katika maeneo mengine wanayopata mradi. Jitumeni acheni uvivu mtafika mbali."

Amesema Serikali inatengeneza ajira kwa vijana kupitia wakandarasi wanaotekeleza miradi, hivyo wakandarasi wanatakiwa wawatumie mafundi wasaidizi walioko kwenye maeneo ya miradi.

Waziri Mkuu amesema amefarijika sana kuona vijana wanapata ajira na amewataka  watumie nafasi hizo kujifunza ufundi ili nao waje kuwa mafundi wakubwa na kuajiri wenzao.

Naye,  fundi msaidizi wa jengo la utawala katika hospitali ya wilaya ya Ruangwa,Hamisi Ali amesema wanaishukuru Serikali kwa kuwapelekea miradi mkubwa ambayo inawapatia ajira.

Ali ametoa wito kwa vijana wengine waache kukaa mitaani na badala yake wajitokeze na wachangamkie fursa za ajira zilizopo kwenye maeneo yao na wafanye kazi hizo kwa bidii.

Waziri Mkuu ametembelea ujenzi wa hospitali ya wilaya, ghala, Ujenzi wa ofisi ya Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Shule ya Seondari ya  Wasichana Lucas Maria.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa hospitali ya Wilaya Ruangwa Machi 16.2019 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na mamantilie Asha Livembe (aliyesimama) na Asha Mluki (kushoto) baada ya kukagua ujenzi wa mradi wa hospitali ya Wilaya Ruangwa Machi 16.2019 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mhandisi Mshauri Edgar Rugemalila, wakati akimuonesha mchoro wa ghala la Wilaya ya Ruangwa kabla ya kukagua ujenzi wa ghala hilo wilayani Ruangwa Machi 16.2019 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mradi wa ujenzi wa ghala wilayani Ruangwa Machi 16.2019 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...