Na. Vero Ignatus, Arusha.

Mamlaka ya Mapato nchini TRA imewataka wafanyabiashara wakubwa mkoani Arusha, kutumia teknolojia za kisasa kwa mtandao kwaajili ya kulipa kodi zao ili kuongeza uwazi na kutunza kumbukumbu zao. 

Wito huo umetolewa na Kaimu Kamishna wa Idara ya walipakodi wakubwa wa TRA, Yeremiah Mbaghi katika warsha ya walipa kodi wakubwa juu ya mifumo ya kulipa kodi na sheria na kanuni mbali mbali za kodi ambazo zimepitishwa na serikali.

Amesema kuwa Matumizi ya mtandao katika malipo ya kodi, yanarahisisha ulipaji wa kodi na yanapunguza gharama kwa wafanyabiashara hao kwenda ofisi ya TRA."TRA imefanya maboresho makubwa katika mfumo wake wa kulipa kodi kupitia mtandao na tumeongeza ufanisi katika utunzaji wa kumbukumbu za kodi ya zuio kwani sasa malipo yote ya kodi zuio hungia moja kwa moja kwenye akaunti ya mlipakodi husika"alisema

Amewataka walipa kodi hao kuzingatia sheria ya fedha ya mwaka 2018 na maboresho ya kanuni, ikiwepo kuwasilisa taarifa za miamala baina yake na washirika kwa kamishna mkuu pale anapowasilisha ritani ya mapato kwa mwaka.

Akifungua warsha hiyo, Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha, Richard Kwitega kwa niaba ya mkuu wa mkoa, Mrisho, Gambo, amesema serikali mkoani Arusha, itaendelea ushirikiana na TRA na walipa kodi ili kuhakikisha mapato ya serikali yanaimarika.

Amesema upatikanaji wa mapato yataiwezesha serikali kutekeleza miradi ya maendelo ambapo serikali ya awamu ya tano imejikita katika kutekeleza miradi endelevu katika kutatua kero za wananchi,kubadili mfumo wa uchumi na kuwa wa kati kwa kukuza sekta ya viwanda.

"kodi ambazo zinalipwa pia zinasaidia sana katika miradi ya huduma za kijamii, maji, barabara, umeme pembejeo na kupatikana huduma bora za afya"alisema.Hata hivyo, amesema kuwa serikali itaendelea kujenga mazingira bora ya biashara nchini, ili kuhakikisha wafanyabiashara wananufaika, serikali inapata kodi na wananchi wanapata mahitaji yao.

Mfanyabiashara Peter Minja alipongeza TRA kuanza kuwatembelea na kutoa elimu juu ya sheria mpya zilizopitishwa na serikali lakini pia juu ya mifumo sahihi ya malipo ya kodi, ikiwepo kodi za mabango.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...