Na Ahmed Mahmoud,Arusha.

Wananchi wa kata ya Lemara eneo la Nanenane jijini Arusha wameamua kujitolea kwa hali na mali kuweka alama za vivuko viwili vya waenda kwa miguu katika barabara inayoingia katikati ya jiji kwenye eneo linalodaiwa kutokea ajali za mara kwa mara na kusababisha watu wasiyo na hatia kupoteza maisha .

Wanahabari walifika kwenye eneo la nanenane na kushuhudia wakazi wa eneo hilo wakichangishana fedha kwa ajili na kuweka alama hizo huku mafundi wakiendelea na kazi ya kuweka alama hizo ambazo zinatajwa kua ni suluhisho la kuzuia ajali kutokea katika eneo hilo.

Wakazi wa kata hiyo wakizungumzia hatua waliochukua ya kujitolea kwa michango yao wakishirikiana na diwani wao nibaada ya eneo hilo kukidhiri ajali za mara kwa mara ambazo wakati mwingine zinaepukika.

Alfredy Maulid na Pascal Silvery ni wakazi wa kata ya lemara walisema upatikanaji wa kivuko hicho ni mkombozi mkubwa hasa watoto wa shule kuvuka kwa amani kwakua kipindi cha nyuma hali ilikua mbaya ya watu kupoteza maisha kwa kugongwa na magari.

Pascal alisema kuwa wanaamini kuwepo kwa alama hizo kutasaidia wanaovuka waweze kuvuka salama hususan wanafunzi ambao hupata adha kubwa wanapotaka kuvuka barabara.

Diwani wa kata ya Lemara Profesa Raymond Mosha alisema kuwa ameungana na wananchi kutokana na umuhimu wa eneo hilo hawezi kuvumilia kuona watu wakiumia wakati wananchi wanaweza kujitoa na kufanikisha jambo hilo .

“Ushirikiano kati ya Wananchi na Viongozi wao umeweza kufanikisha jambo hili muhimu ,tayari tulishatoa taarifa uongozi wa Jiji umetoa ridhaa kwa wananchi kufanya jambo hili hivyo lina Baraka zote za jiji” Alisema Profesa Mosha

Dereva wa magari Johnson Mlay alisema hatua iliyofanywa na wananchi itawasaidia kufuata sheria ili kuepusha ajali zisizo za lazima.
Mafundi wakiweka alama za vivuko barabarani katika eneo la Nane nane jijini Arusha baada ya Wananchi kata ya Lemara kuchangia zoezi hilo ambalo limefanyika kwa kushirikiana na Wataalamu kutoka Jiji la Arusha ili kuzuia ajali za barabarani hususan kwa wanaopita kwa miguu. Picha na Mahmoud Ahmad Arusha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...