Na.Khadija seif,Globu ya jamii

KAMPUNI ya Multichoice nchini kupitia king'amuzi cha Dstv imechezesha droo ya tatu ya promosheni ya tia vitu upate vituuzi jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari  leo jijini Dar,Mkuu wa kitengo cha thamani kwa wateja Hilda Nakajumo wakati wa kutangaza washindi hao 15 waliopatikana katika kila vifurushi kama Compakt plus,family , premier pamoja na kifurushi cha bomba amesema ni wakati wa wateja kunufaika,kufaidika na kuendelea kuuwasha moto kiburudani zaidi.

"Leo tumefanikiwa kupata washindi 15 kutoka mikoa mbalimbali kama vile Arusha ,Kagera,Manyara pamoja na Dar es salaam inaonyesha wazi king'amuzi cha dstv kinaendelea kutoa huduma nzuri na gharama nafuu,alisema nakajumo"

Aidha amesema washindi hao wamezawadiwa malipo ya miezi miwili bure ili kuendelea kufaidika na vipindi mbalimbali kupitia King'amuzi cha dstv.

Hata hivyo kwa upande wake Afisa Mwandamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha Humud Abdulhussein amesema ni wakati wa wateja wa dstv kulipia ving'amuzi vyao kwa wakati ili kupata ofa hiyo ."Hakuna mtu ambae anapangwa droo inachezeshwa kwa haki bila janja yoyote pamoja na vigezo na masharti vinazingatiwa ipasavyo ," alisema Abdulhussein.

Na Mshindi wa kifurushi cha Compart mkazi wa jijini Mwanza Musa juma mwenye umri wa miaka 24 amewapongeza dstv kwa promosheni hiyo ya tia vitu pata vituuz."Sikutegemea kama ningeweza kushinda katika droo hii ya 3 mara nyingi nasikia tu wenzangu wakishinda nikajaribu bahati yangu na nikaamua kulipia kwa wakati king'amuzi changu hatimae nimeibuka mshindi," alisema juma

Pia amewapa ujasiri wateja wengine kulipa kwa wakati ili waweze kuingia kwenye droo hiyo na kushinda kabisa.Mkuu wa kitengo cha thamani kwa wateja kampuni ya Multichoice kupitia king'amuzi cha Dstv Hilda Nakajumo akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza washindi 15 waliopatikana katika droo ya 3 ya promosheni ya tia kitu pata vituuz akiwa pamoja na Afisa Mwandamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha Humud Abdulhussein .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...