Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (katikati) akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhe. Mtemi Simeoni (kushoto) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea Shamba la Miti la Biharamulo mara baada ya kukagua maendeleo ya miti iliyopandwa katika shamba hilo kwa ukubwa wa hekari 900 katika wilaya ya Chato mkoani Geita., Kulia ni Meneja wa shamba hilo, Edward Nyondo.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhe. Mtemi Simeoni (kushoto) alipotembelea Shamba la Miti la Biharamulo mara baada ya kukagua maendeleo ya miti iliyopandwa katika shamba hilo kwa ukubwa hekari 900 katika wilaya ya Chato mkoani Geita. Wengine ni watumishi pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na wananchi pamoja na watumishi wa shamba la miti la Biharamulo ambalo mara baada ya kukamilika kwa kupandwa miti katika eneo lote litakuwa ndio shamba la pili kwa ukubwa kati ya mashamba 20 yanayomilikiwa na Wakala wa Hudumza Misitu Tanzania lililopo wilayani Chato mkoani Kagera.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akipanda mti wakati alipotembelea Shamba la Miti la Biharamulo mara baada ya kukagua maendeleo ya miti iliyopandwa katika shamba hilo lenye ukubwa wa hekari 900 katika wilaya ya Chato mkoani Geita

Mkuu wa wilaya ya Chato, Mhe. Mtemi Simeoni akipanda mti wakati alipoambatana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu alipotembelea Shamba la Miti la Biharamulo mara baada ya kukagua maendeleo ya miti iliyopandwa katika shamba hilo lenye ukubwa wa hekari 900 katika wilaya ya Chato mkoani Geita
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa wilaya na watumishi wa Shamba la Miti la Biharamulo lililopo katika wilaya ya Chato mkoani Geita.
Baadhi ya watumishi wa Shamba la Miti la Biharamulo wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja katika shamaba hilo hukuakiwasisitizan umuhimu wa kufanya kazi kwa kushirikiana na wananchi wanaoishi karibu na shamba hilo.
(Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii)
…………………………. 

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ametoa muda wa miezi mitatu kwa wananchi waliovamia na kuanzisha shughuli za kibinadamu ndani ya Shamba la miti la Biharamulo kuondoka mara moja kwa hiari yao bila shuruti kabla ya mwezi Juni mwaka huu. 

Ametoa muda huo ili wananchi waliolima mazao mbalimbali yakiwemo mahindi na pamba waweze kuvuna mazao yao kabla ya kuanza kwa oparesheni maalum ya kuwaondoa, iliyopangwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi Julai mwaka huu itakayofanywa na Wakala wa Huduma ya Misitu Tanzania ( TFS) kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo. 

Mhe.Kanyasu ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutembelea shamba la miti Biharamulo lililopo katika wilaya ya Chato mkoani Geita.
Amesema Oparesheni hiyo haitasubiri taarifa ya Wizara tano inayoendelea kufanyiwa kazi kwa kuwa eneo hilo halihusiani na vile vijiji 366 vilivyokutwa ndani ya Hifadhi. 

Amesema haiwezekani wananchi waliovamia eneo hilo waendelee kuachwa kwa kisingizio cha Kauli ya Rais aliyoitoa Januari 15 mwaka huu kuhusiana na vijiji 366 vilivyokutwa ndani ya maeneo ya Hifadhi. 

Amebainisha kuwa wananchi waliovamia eneo hilo wameitafsiri visivyo Kauli hiyo na kuongeza kuwa baada tu ya tamko la Mhe. Rais , baadhi ya wananchi hata wale waliokuwa wakiishi katika maeneo mengine nje ya hifadhi waliendelea kuvamia na kuanza kujimilikishia maeneo makubwa wakidai kuhalalishwa na tamko la Rais. 

Amefafanua kuwa taarifa inayoendelea kufanyiwa kazi na timu ya Mawaziri na Makatibu Wakuu kutoka Wizara tano imebainisha kuwa mpaka sasa zaidi ya vijiji 700 vimekutwa ndani ya Hifadhi badala 366 vilivyoripotiwa awali. 

Kufuatia hali hiyo amesema baadhi ya wavamizi wa Hifadhi katika maeneo mbalimbali wataendelea kuondolewa bila kusubili kukamilika kwa zoezi linaloendelea kwa kuwa walieendelea kuvamia maeneo ya Hifadhi kwa kisingizio cha tamko la Rais huku maeneo hayo yakizidi kuharibiwa kwa miti kukatwa na shughuli nyingi za kibinadamu 

Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu ameiagiza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) kutenga Bajeti ya kugharamia operesheni ya kuwaondoa wavamizi ndani ya Shamba hilo. Ameitaka TFS kuendesha oparesheni za mara kwa mara ili wavamizi hao wajue Serikali ipo kazini kulinda rasilimali za Taifa muda wote. 

Awali, Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mtemi Simeoni akizungumza katika ziara hiyo alisema kuwa baadhi ya wananchi kutoka nje ya wilaya hiyo wamekua wakivamia na kuanzisha shughuli za kibinadamu ndani ya Shamba hilo, suala ambalo ni kinyume cha sheria. 


Mkuu huyo wa wilaya amebainisha kuwa wananchi katika maenro hayo wana mahitaji makubwa ardhi na kuiomba Wizara iangalie namna ya kuwasaidia hekari 5000 ili wapate maeneo ya kulima na kuchungia mifugo yao.
Kwa upande wake Meneja wa Shamba hilo Bw. Thadeus Shirima amemweleza Naibu Waziri huyo kuwa hadi sasa zaidi ya hekari 900 zimepandwa miti licha ya Shamba hilo kukabiliwa na changamoto ya uhaba wa watumishi pamoja na vitendea kazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...