Waziri wa Madini Doto Biteko amekutana na Rais wa Kampuni ya Amtec Resources Management Ltd ya nchini Uingereza, Dkt. Peter Gollmer ambaye amemweleza Waziri Biteko kuhusu ujio wa kampuni zipatazo 3 kutoka mataifa mbalimbali zenye nia ya kuwekeza katika sekta ya madini.

Dkt. Gollmer amesema kampuni hizo zimeonesha nia ya kuwekeza katika sekta ya madini hususan katika masuala ya utafiti na uchimbaji wa madini kutokana na ushawishi unaofanywa na Balozi wa Tanzania nchini Urusi Meja Jenerali Mstaafu Simon Mumwi  ambaye amekuwa akihamasisha watu wa mataifa mbalimbali nchini humo kuwekeza nchini.

Pia, ameeleza kwamba, kampuni hizo hazina shaka ya kuwekeza Tanzania kutokana na mazingira tulivu ya kisisasa yaliyopo nchini pamoja na utajiri wa rasilimali madini ambayo Tanzania imejaliwa kuwa nayo.
Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Biteko amemweleza Dkt. Gollmer kuwa kikao hicho ni muhimu na kwamba milango kwa ajili ya wawekezaji wenye dhamira ya dhati ya kuwekeza nchini iko wazi na kuongeza kuwa, kama wizara inaratajia kukutana na kampuni hizo.

Wengine walioshiriki kikao hicho ni Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa, Mkurugeni wa Idara ya Sera na Mipango, Augustine Ollal na Katibu wa Waziri Kungulu Kasongi.
 Waziri wa Madini Doto Biteko akimsikiliza Rais wa Kampuni ya Amtec Resources Management Ltd ya nchini Uingereza, Dkt. Peter Gollmer.
Kamishna wa Madini David Mulabwa akizungumza jambo wakati wa kikao baina ya Waziri wa Madini Doto Biteko na Rais wa Kampuni ya Amtec Resources Management Ltd ya nchini Uingereza, Dkt. Peter Gollmer
Waziri wa Madini Doto Biteko akizungumza jambo na Rais wa Kampuni ya Amtec Resources Management Ltd ya nchini Uingereza, Dkt. Peter Gollmer. Anayefuatilia ni Mkurugenzi wa Ssera na Mipango Wizara ya Madini, Augustine Ollal.
Waziri wa Madini Doto Biteko akiteta jambo na Rais wa Kampuni ya Amtec Resources Management Ltd ya nchini Uingereza, Dkt. Peter Gollmer. Kulia wanaofuatilia ni Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa na Katibu wa Waziri, Kungulu Kasongi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...