Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Ujenzi na Ukarabati Mkubwa wa Kituo cha Afya cha Koromije wilayani Misungwi Machi 19, 2019. Kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa, wa pili kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Misungwi, Gambadu Samwel.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia baada ya kukata utepe ikiwa ni ishara ya kufungua Ujenzi na Ukarabati Mkubwa wa Kituo cha Afya cha Koromije wilayani Misungwi, Machi 19, 2019. Wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Misungwi, Juma Sweda na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Misungwi, Samwel Gambadu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe ikiwa ni ishara ya kufungua Ujenzi na Ukarabati Mkubwa wa Kituo cha Afya cha Koromije wilayani Misungwi, Machi 19, 2019. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Misungwi, Juma Sweda na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Misungwi, Samwel Gambadu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Grace Fabian aliyejifungua mtoto wa kiume katika Kituo cha Afya cha Koromije wilayani Misungwi wakati alipofungua Ujenzi na Ukarabati Mkubwa wa Kituo hicho, Machi 19, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefungua mradi wa ujenzi na ukarabati mkubwa wa kituo cha afya cha kata ya Koromije wilayani Misungwi na amewahakikishia wananchi kuwa Serikali imejipanga vizuri kuboresha huduma za afya.

Amesema uboreshaji huo unahusisha ujenzi wa chumba cha upasuaji, maabara, chumba cha kujifungulia, wodi ya mama na mtoto na wodi ya wanawake na wanaume pamoja na chumba cha kuhifadhia maiti.Uboreshaji huo unagharimu sh. milioni 500.

Waziri Mkuu alifungua mradi huo jana (Jumanne, Machi 19, 2019) akiwa ziarani Misungwi, ambapo aliwataka wananchi waendelee kuiunga mkono Serikali yao, ambayo imedhamiria kuwatumikia ili waweze kupata maendeleo.

“Hapa zamani kulikuwa na zahanati yenye jengo moja, tumeamua kuboresha na kupandisha hadhi na kuwa kituo cha afya. Rais Dkt. John Magufuli anataka wananchi wapatiwe huduma muhimu zikiwemo za afya karibu na makazi yao”.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alisema hakuna kijiji chochote nchini kitakachoachwa bila ya kuunganishiwa umeme katika awamu ya tatu ya Mradi wa Nishati Vijijini (REA), vikiwemo na vya wilaya ya Misungwi tena kwa gharama nafuu.

“Rais wetu Dkt. John Magufuli anajali sana wananchi wake, hivyo ametenga fedha nyingi zitakazotosheleza kusambaza umeme katika vijiji vyote vikiwemo na wilaya yenu hii ya Misungwi. Gharama za kuunganishiwa umeme huo ni sh. 27,000 tu.”

Waziri Mkuu aliongeza kwamba lengo la Serikali ni kufikisha umeme kwenye vijiji vyote Tanzania na vile ambavyo viko kwenye maeneo yaliyo mbali na gridi ya taifa vitafungiwa sola, jambo ambalo litafungua fursa za ajira na kukuza uchumi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...