Mbunge wa Viti Maalum anayewakilisha vijana bungeni, Zainabu Katimba, kulia, akizungumza na baadhi ya vijana wanaowakilisha makundi mbalimbali jijini Dar es Salaam, katika kongamano aliloandaa lenye dhamira ya kuangalia fursa za kiuchumi zinazoweza kufanyia na vijana kwa ajili ya kukuza uchumi wao. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Friedrich Ebert Stiftung (FES), Andreas Quasten, ambayo wameshirikiana na Mbunge kuwezesha Kongamano hilo. Picha na Mpigapicha Wetu.

Mbunge wa Viti Maalum anayewakilisha vijana bungeni, Zainabu Katimba, akizumgumza na waandishi wa habari hawapo pichani katika kongamano aliloandaa lenye dhamira ya kumuwezesha kijana katika hali ya kufanyia kazi changamoto zinazowakabili vijana nchini Tanzania. Kongamano hilo pia limeandaliwa kwa ushirikiano mkubwa wa taasisi ya Friedrich Ebert Stiftung (FES). Picha na Mpigapicha Wetu. 


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam 

VIJANA mbalimbali nchini Tanzania, wameaswa kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi, ikiwamo namna bora ya kuungana vikundi ili kuomba fedha za Halmashauri ambazo zimekuwa zikikosa waombaji katika maeneo mengi, huku sababu kubwa ni uelewa mdogo juu ya upatikani wa fedha hizo zinazotolewa maalum ili kuwakomboa vijana kiuchumi. 

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Viti Maalum, akiwakilisha vijana katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Zainabu Katimba, katika kongamano la vijana aliloandaa kwa kushirikiana na taasisi yake ya WEZESHA, akishirikiana pia na Taasisi ya Friedrich Ebert Stiftung, ikikutanisha viongozi wa makundi mbalimbali jijini Dar es Salaam, nchini hapa. 

Akizumgumzia changamoto hizo, mheshimiwa Katimba alisema kuwa wapo watu wanaoamini kuwa fedha hizo hazipo au zinatoka kwa watu maalum, bila kujua kwamba fedha hazitoki kwa watu mmoja mmoja na kinachotakiwa ni kuungana katika makundi na kuanisha vipengele vya kimkakati, jambo ambalo limekuwa halifanyiki. 

“Mimi nawakilisha vijana kule bungeni, lakini pia tunaelekea kwenye bajeti mpya, hivyo naamini pamoja na mambo mengine, tukitoka kwenye kongamano hili la kuwezesha a, kuelimishana sambamba na kufungua milango ya kuiona fursa, naamini tutakuwa katika nafasi nzuri, zaidi uwezo wa vijana kuzichangamkia pia fedha za serikali katika Halmashauri zetu. 

“Nimekuwa nikifanya makongamano haya kwa muda mrefu na dhamira yetu kubwa ni sisi vijana wenyewe kujitambua, kwa sababu tunapoweza kutumia fursa tunazokutana nazo mtaani, walau tunaweza kujikwamua kiuchumi na kulikomboa pia Taifa letu ambalo sera ya viwanda imeshika kasi na sisi vijana wenyewe ndio nguvu kazi ya Taifa kwa namna moja ama nyingine,”Alisema Katimba, ambaye pia ni mwasisi wa taasisi ya Wezesha. 

Akizumgumzia kongamano hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Friedrich Ebert Stiftung (FES), Andreas Quasten, alimpongeza Mbunge wa Viti Maalum, Zainabu, kwakuwa karibu na vijana akisema anawawakilisha vizuri bungeni.
“FES tunampongeza bi Zainabu kwa kufanya mambo mengi yanayohusu vijana, ambapo tunaamini kwa uwapo wake bungeni, unasaidia kuwezesha vijana, katika kipindi hiki ambacho idadi kubwa ya watu Tanzania ni vijana, huku wakiwa na changamoto nyingi ikiwamo ajira, ushiriki katika mambo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi. 

“Sisi FES tutaendelea kushirikiana na makundi yote sambamba na serikali Kuu ili kuhakikisha kwamba changamoto hizo zinakwisha ili kuwafanya vijana na Watanzania wote wanaishi maisha vizuri, sanjari na uelewa mpana wa kutumia fursa endelevu za kiuchumi,”Alisema. 


Katika kongamano hilo la siku moja lililofanyika katika ofisi Kuu za FES zilizopo Kinondoni, Morocco, jijini Dar es Salaam, vijana mbalimbali walichambua changamoto wanazokutana nazo mitaani, bila kusahau mwelekeo unaoatakiwa kufuatwa katika Bajeti Kuu ya Serikali itakayosomwa baadaye mwaka huu bungeni, jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...