Binti mwenye umri wa miaka 19 mkazi wa Wilaya ya Urambo amejeruhiwa vibaya sehemu ya Tumboni baada ya Kuchomwa Kisu na Msichana mwenzake Chanzo ikiwa ni Wivu wa mapenzi 


Tukio hili limetokea katika mnada wa kitongoji cha mwenge kata ya Urambo mjini likimuhusisha mmoja anayetajwa kwa jina la Kalunde Madua mwenye Umri wa miaka 20 baada ya kumchoma mwenzake Joyce Isaya kwa kile kinachodaiwa ni wivu wa mapenzi na kumshuku kuwa anatoka na mvulana wake 

Baada ya tukio hilo Kalunde alishambuliwa na Wananchi waliokuwepp kwenye eneo hilo na kupelekwa kituo cha polisi huku Joyce akikimbizwa Hospitali  ya Wilaya ya Urambo

Kwa mujibu wa Mama yake mzazi na Joyce bi. Cesilia Mathias alipozungumza na Michuzi Blog akiwa katika hodi aliyolazwa Mwanae Joyce amesema

"Ugomvi baina ya binti yangu Joyce na Kalunde ulianza zamani Licha ya wazazi na Majirani Kujaribu kuwakalisha kikao cha kuwasuluhisha Lakini bado wameendelea kuhitalafiana mara kadhaa 

Mganga Mkuu Wa Wilaya Ya Urambo Paul Swakala amekili kumpokea Mgonjwa huyo na kuongeza kuwa 

"Baada ya kuwa amechomwa Kisu sehemu ya kushoto ya tumbo kwa baahati nzuri Kisu hakikuweza kuingia ndani hivyo anaendelea na matibabu mpaka sasa  tunaendelea na uchunguzi wa kina kuhakikisha anapata nafuu na bado yupo chini ya uangalizi wa Hospitali "Amesema Swakala

Naye Mwenyekiti wa kitongoji cha msufini kata ya Kapilula Bw. Lameck Zakayo ameiomba Serikali kumchukulia hatua kali za kisheria na watu wenye tabia kama  hizo 

Hata hivyo kwa mujibu wa Daktari Swakala amesema binti huyo aliyejeruhiwa atapatiwa ruhusa hivi karibuni kutokana na majereha yake kutokuwa ya kutisha na kwa upande wa Kalunde bado anashikiliwa na jeshi la polisi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...