Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAKATI kesho ya Aprili 9,mwaka huu Chama cha ACT Wazalendo kikitarajia kufanya maandamano makubwa ,tayari Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limesema limejipanga kukabiliana na waandamanaji hao na iwapo watajitokeza watapigwa mkapa watachakaa.

Akizungumza leo Aprili 8,2019, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto amesema kuwa kupitia mitandao ya kijamii kuna taarifa za ACT Wazalendo kutaka kufanya maandamano kwa kushirikiana na baadhi ya vyama vingine kikiwemo Chama cha NCCR-Mageuzi.

"ACT Wazalendo wanakusudia kufanya maandamano kesho yaani Apirili 9,2019. Nataka kuwaambia hao wanaotangaza maandamano kwa njia ya mtandao wakiingia barabarani kama ni kweli watapigwa watachaa.Narudia tena watapigwa watachakaa,"amesema Kamanda Muroto .

Amefafanua Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kwa sasa linaendelea na mazoezi na lipo tayari kukabiliana na wandamanaji, hivyo wanawasubiri kwa hamu kama wapo huku akifafanua maandamano hayo ni haramu na hayapaswi kufanyika.

"Wananchi wa Mkoa wa Dodoma msiwe na wasiwasi, endeleeni na shughuli zenu kama kawaida na wabunge nao waendelee na vikao vya Bunge.Polisi tumejipanga na tuko tayari,"amesema Kamanda Muroto na kusisitiza watakaondamana hiyo kesho watapigwa watachaa.

Kwa kukumbusha tu, ACT Wazalendo walitangaza kufanyika kwa maandamano hayo ikiwa ni sehemu ya kuonesha hisia zao za kutofurahishwa na uamuzi wa Bunge la kutofanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) Profesa Mussa Assad

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...