Shirika la Agape ACP limetoa elimu ya kutambua haki za binadamu ili kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana wafanyabiashara katika soko la Ngokolo Mitumbani Manispaa ya Shinyanga. 

Elimu hiyo imetolewa leo Jumamosi Aprili 13,2019 wakati Mnada wa Jumamosi katika Soko la Ngokolo Mitumbani ukiendelea hivyo kufanikiwa kuwafikia watu mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara na wananchi waliofika mnadani hapo kujipatia mahitaji yao. 

Agape ACP wanatoa elimu ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na wasichana wafanyabiashara sokoni ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa “Mpe Riziki Si Matusi” unaofadhiliwa na shirika la UN WOMEN kupitia Shirika la kitaifa la Equality for Growth (EfG). 

Akitoa elimu, Meneja Miradi wa shirika la Agape, Mustapha Isabuda aliwataka wanawake na wasichana wanaofanyiwa vitendo vya kikatili kwenye masoko na katika jamii kwa ujumla kuacha tabia ya kuwa wakimya na badala yake watoe taarifa kwa viongozi mbalimbali ikiwemo Dawati la Jinsia katika kituo cha polisi. 

“Acheni kukaa kimya mnapofanyiwa ukatili,msikubali kukaa na makovu ya ukatili kwenye masoko,pazeni sauti zetu,nanyi wanaume acheni kunyanyasa wanawake,msiwatukane na msiwadhulumu mama lishe,wapeni riziki si matusi”,alieleza Isabuda. 

Isabuda alitumia fursa hiyo kuikumbusha jamii kuthamini wanawake na wasichana wafanyabiashara sokoni huku akiwatahadhalisha wanaume kuwa waaminifu katika ndoa zao na kuacha tabia ya kutongoza na kufanya mapenzi na wanafunzi kwani matokeo yake ni kufungwa jela miaka 30. 

Naye Afisa Mradi wa 'Mpe Riziki Si Matusi' kutoka Agape,Helena Daudi alisema Agape imeendelea kutoa elimu katika masoko mbalimbali katika Manispaa ya Shinyanga ikiwemo Soko Kuu,Kambarage,Nguzo Nane Ngokolo Mitumbani na Majengo Mapya ili jamii iachane na tabia ya kuwafanyia ukatili wanawake na wasichana wafanyabiashara 

Alisema tayari wamewajengea uwezo wasimamizi wa sheria ili wakaosaidia kutokomeza ukatili wa kijinsia unaotokea kwenye masoko. 

Naye Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Soko la Ngokolo Mitumbani,Tracy Leonard alisema wafanyabiashara wanaofanyiwa zaidi ukatili sokoni akina mama hususani mama lishe ambao wanatolewa lugha chafu,wanadhulumiwa na kufanyiwa mashambulio ya aibu ikiwemo kushikwa shikwa bila idhini yao. 

Alizitaja hatua ambazo wamekuwa wakizichukua pindi panapotokea ukatili sokoni kuwa ni kusuluhisha,kuwapiga faini ya shilingi 5000 wanaotukana na kama ni mfanyabiashara basi akirudia kutukana basi hufungiwa biashara yake kwa muda wa wiki mbili.
Meneja Miradi wa shirika la Agape, Mustapha Isabuda akitoa elimu ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana wafanyabiashara katika soko la Ngokolo Mitumbani leo - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Meneja Miradi wa shirika la Agape, Mustapha Isabuda akielezea madhara ya kuwafanyia ukatili wanawake na wasichana wafanyabiashara sokoni.
Wananchi wakimsikiliza Isabuda.
Meneja Miradi wa shirika la Agape, Mustapha Isabuda akiwasisitiza wanaume na wanawake kuacha kuwafanyia ukatili wanawake na wasichana wafanyabiashara sokoni.
Wananchi wakimsikiliza Isabuda.
Afisa Mradi wa Mpe Riziki Si Matusi kutoka Agape,Helena Daudi akiwahamasisha wananchi kuwapenda wanawake na wasichana wafanyabiashara sokoni badala ya kuwanyanyasa na kuwanyima haki zao.
Afisa Mradi wa Mpe Riziki Si Matusi kutoka Agape,Helena Daudi akiwataka wanawake kutoa taarifa pale wanapofanyiwa ukatili.
Wananchi wakisoma vipeperushi mbalimbali vya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na wasichana wafanyabiashara sokoni.
Wananchi wakiwa eneo la tukio.
Kikundi cha burudani cha 'Shinyanga Arts Group' kinachoongoza na Msanii ChapChap kikitoa burudani.
Burudani inaendelea.
Wasaidizi wa Kisheria kwenye masoko waliopewa mafunzo na Agape ACP wakitoa eimu ya kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake na wasichana wafanyabiashara kwenye masoko. Aliyeshikilia kipaza sauti kulia ni Shangwe Omary.
Msaidizi wa Kisheria sokoni, Asha Jumanne akitoa elimu kwa jamii namna ya kutokomeza ukatili wa kijinsia kwenye masoko.
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Soko la Ngokolo Mitumbani,Tracy Leonard akielezea jinsi wanavyokabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na wasichana wafanyabiashara sokoni ambapo wamekuwa wakipiga faini ya shilingi 5000 wanaotukana na kufunga biashara za wafanyabiashara wanaofanya ukatili sokoni.
Katibu wa Wafanyabiashara Soko la Ngokolo Mitumbani,Tracy Leonard akielezea namna wanavyowatetea akina mama wanaofanyiwa ukatili sokoni.
Mfanyabiashara Soko la Ngokolo Mitumbani,Zuhura Athuman akielezea changamoto wanazokutana nazo sokoni ikiwemo kutolewa lugha chafu.


Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...