Dereva wa gari dogo aina ya Nissan March lenye namba za usajili T968 DNZ amefariki dunia baada ya gari hilo kugongana na Basi la Mwendokasi eneo la Magomeni Mapipa jijini Dar es salaam mchana wa Ijumaa Kuu. 

Kwa mujibu wa mashuhuda, basi la mwendokasi lilikuwa likitoka maeneo ya Kariakoo kwenda Kimara, kabla ya kuligonga gari hilo dogo ambalo liliklatika katikati huku dereva wake akifariki dunia papo hapo.

Shuhuda wanasema mwenye gari dogo alikuwa anakata kona kutoka Magomeni kwenda Kariakoo, sasa wakati anataka kuikata kona katika taa ndogo za kuongoza magari za Magomeni Mapipa ambazo zilikuwa haziwaki ndipo gari dogo ikachelewa kupita na mwendokasi likawa limefika na kuligonga.
Vipande viwili vya gari hilo vimechukuliwa na kupelekwa kituo cha Polisi Magomeni huku mwili wa dereva huyo ambaye haujafahamika jina lake umepelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...