Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) wamezindua rasmi mchakato wa kumtafuta mwajiri bora kwa mwaka 2019 lengo likiwa ni kutambua na kutoa tuzo kwa Waajiri wenye misingi bora ya usimamizi wa nguvu kazi na rasilimali watu ili kuwawezesha kutimiza wajibu wao kwa ajili ya kuongeza uzalishaji kibiashara.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa ATE Dkt. Aggrey Mlimuka alisema kwamba Tuzo ya mwajiri bora wa mwaka (EYA) ni zoezi lililoanzishwa na kuendeshwa kila mwaka na Chama cha Waajiri Tanzania tangu mwaka 2005 ambapo Tuzo za mwaka huu pia zimepanuka sio tu kujali rasilimali watu bali pia kutambua Waajiri wanaofuta taratibu za kitaifa na kimataifa katika uendeshaji wa biashara zao.

“Ushiriki wa Tuzo ya Mwajiri Bora umeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka kutokana na ukweli kuwa waajiri wengi wamehamasishwa kuthamini watu katika kufanikisha shughuli za biashara kama nyanja muhimu ya usimamizi wa rasilimali watu mahali pa kazi” Alisema Dkt. Mlimuka. 

Akielezea zaidi kuhusu tuzo ya mwaka huu 2019, Dkt. Mlimuka alisema kuwa Kutokana na maoni waliyopokea kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, wadau na wataalamu wetu mbalimbali, tuzo ya mwajiri bora kwa mwaka huu 2019 imekuja na vipengele vipya vitatu (3) na kufanya kuwa na Jumla ya vipele 38 kutoka vipengele 35 vilivyokuwepo awali na.

Dkt Mlimuka amevitaja vipengele vilivyoongezeka kuwa ni Mwajiri Bora anaeendaleza Mafunzo ya Ujuzi wa Kazi kwa wahitimu (Internship),Mwajiri Bora anayetoa mafunzo ya Uanagenzi (Apprentiship) na Mwajiri Bora anayezingatia Haki Rasilimali (Local Content)

“Lengo la kuongeza vipengele hivi ni kuendelea kuziboresha tuzo hii na kuongeza ushindani miongoni mwa washiriki na pia kujaribu kugusa kila eneo ambalo litaleta tija katika ukuzaji na uendelezaji wa rasilimali watu katika maeneo ya kazi.” Alisema Dkt. Mlimuka.

Dkt. Mlimuka aliendelea kwa kusema kuwa Tuzo hizo mpya zitakuwa ni nyongeza ya zile ambazo zimekuwa zikitolewa katika masuala ya utawala na uongozi, ubora katika usimamizi wa rasilimali watu, bidhaa au huduma, uzalishaji na ubunifu, uwajibikaji katika mwenendo wa biashara, utendaji unaokidhi, ushirikishwaji wa mwajiriwa, ukuzaji wa vipaji, mafunzo na maendeleo pamoja na usalama wa mwajiriwa katika mazingira ya kazi. 

Tuzo nyingine ni ile  ya uwiano wa kazi na maisha,  mwajiri bora ni yule anayesimamia vema nguvu kazi inayoonekana kupotea/kupuuzwa, Waajiri bora wenye mikakati inayojali afya za waajiriwa, tuzo ya utofautishwaji na ushirikishwaji yaani (diversity and inclusion), Waajiri bora waonaowachochea na kuwajali waajiriwa wenye ujuzi, Waajiri bora wenye mahusiano mazuri baina ya waajiri na waajiriwa, Waajiri bora wenye majina makubwa na imara huvutia wateja, waajiriwa, wadau na mwajiri bora aliyewekeza kwenye teknolojia.

“Pia tutaendelea kuwa na Tuzo ya Mshindi wa Jumla (Overall) na tuzo kulingana na ukubwa, nazo ni zile zinazohusu tuzo ya waajiri bora katika sekta binafsi, sekta za umma pamoja na mashirika ya ndani ya nchi.” Alielezea Dkt. Mlimuka.

Dkt. Mlimuka pia alitumia siku hiyo kuwaarifu waajiri kuwa kitabu cha Mwongozo wa Misingi Muhimu ya Kusimamia Rasilimali Watu ya Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka kipo tayari hivyo kuwaomba waajiri wote waweze kujipatia mwongozo huu utakaoelekeza makampuni mambo ya kuzingatia katika usimamizi wa rasilimali watu ili kuongeza tija na kuongeza ushindani.

 Mchakato wa kumpata Mwajiri Bora wa Mwaka huwa na sehemu mbili; sehemu ya kwanza ni ya utafiti itakayopelekea kupata washindi na kwa sasa sehemu hiyo ipo chini ya kampuni binafsi, TanzConsult inayoongozwa na Prof. BAT Kundi na sehemu ya pili ni usimamizi wa matukio mpaka kilele cha sherehe ambacho kimepangwa kufanyika mapema mwezi Desemba 2019.  

Hivi wanachama waajiri watatarifiwa kutembelea tovuti maalumu kwa tuzo hizi www.eya.co.tz kwa ajili ya kujua Zaidi jinsi ya kushiki. Mwaka huu pia tumeamua kuanza mchakato huu mapema Zaidi ili kuwapa Waajiri wengi muda wa kujiandaa.
Mkurugenzi Mtendaji wa ATE Dkt. Aggrey Mlimuka akizungumzia uzinduzi wa mchakato wa kumtafuta mwajiri bora kwa mwaka 2019 lengo likiwa ni kutambua na kutoa tuzo kwa Waajiri wenye misingi bora ya usimamizi wa nguvu kazi na rasilimali watu ili kuwawezesha kutimiza wajibu wao kwa ajili ya kuongeza uzalishaji kibiashara. Kulia ni Msimamizi wa Mchakato huo kutoka Kampuni binafsi ya TanzConsult Prof. BAT Kundi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...