Benki ya Exim leo imezindua kampeni maalum inayofahamika kama 'Afconika na Exim' ambayo inatoa fursa kwa wateja wa benki hiyo kulipiwa gharama zote za safari na malazi ili waweze kushuhudia mechi za timu ya taifa, Taifa Stars katika mashindano ya fainali za Kombe la Mataifa ya Africa (Afcon) 2019 nchini Misri.

Akizungumza wakati wa unzinduzi wa kampeni hiyo jijini Dar es Samaam leo, Mkuu wa huduma ya rejareja wa benki ya Exim, Bw. Andrew Lyimo alisema kampeni hiyo ya miezi miwili itakamilika mwanzoni mwa mwezi Juni na ipo wazi kwa wateja wapya na wale ambao tayari wana akaunti za benki hiyo.

“Kampeni hii inakuja ikiwa ni mwendelezo wa mkakati wa benki ya Exim katika kusimamia ustawi wa wateja unaofahamika kama 'Exim kazini leo, kwa ajili ya kesho' (Exim at Work Today, for tomorrow) unaoendana na dira na muelekeo wa benki hiyo. Ni kampeni inayothibitisha nia ya benki ya Exim katika kutafuta kesho iliyo bora kwa wateja na jamii inayoizunguka.’’ Alisema.

Alisema washindi wa kampeni hiyo watapata fursa ya pekee ya kufurahia mchezo wanaoupenda huku pia wakipata fursa ya kuungana na Taifa Stars katika mashindano hayo huku wakiwa wamelipiwa gharama zote za safari ikiwemo gharaza na Visa, tiketi ya ndege, gharamza za tiketi ya kushuhudia mechi hizo pamoja na fedha za kujikimu.

"Jumla kutakuwa na washindi watano ambapo washindi wawili watapatikana katika mwezi wa awali wa kampeni na washindi wa wengine watatu watapatikana katika mwezi wa mwisho wa kampeni hii.’’ Alisema.

Kwa mujibu wa Bw. Lyimo ili kushiriki katika kameni hiyo, wateja wapya wanapaswa kufungua Akaunti ya Akiba na kuhakikisha kila mwezi ina kiasi kisichopungua Tshs 500,000 au zaidi au kufungua Akaunti ya Current/biashara ikiwa na wastani wa kila mwezi wa Tshs 10,000,000 au hifadhi ya amana maalum (Fixed deposit) yenye thamani isiyopungua Tshs 5,000,000. "Alisema.

Kwa wateja ambao tayari wana akaunti ya benki hoyp, Bw Lyimo alisema wanachotakiwa kufanya ni kuongeza akiba kwa kiasi cha Tshs 500,000 au zaidi kwa Akaunti za Akiba au kuongeza kiasi cha Tshs 10,000,000 kwenye akaunti zao za Current/biashara au kuwa na hifadhi ya amana maalum (Fixed deposit) yenye thamani isiyopungua Tshs 5,000,000.

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim, Stanley Kafu, alisema kampeni hiyo ni fursa adimu ambapo itatoa nafasi kwa washindi hao kuweza kushuhudia Taifa Stars ikitimiza ndoto zake za kushiriki katika mashindano ya AFCON baada ya zaidi ya miaka 30 kupita.

Kwa mujibu wa Bw Kafu, kampeni hiyo ni sehemu ya mkakati wa kibenki katika kutafuta kesho bora kwa wateja wake na jamii kwa ujumla ambapo pamoja na mambo mengine benki hiyo imekuwa ikiunga mkono agenda za kitaifa ikiwemo suala zima la michezo.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim, Stanley Kafu (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kampeni maalum inayofahamika kama 'Afconika na Exim' ambayo inatoa fursa kwa wateja wa benki hiyo kulipiwa gharama zote za safari na malazi ili waweze kushuhudia mechi za timu ya taifa, Taifa Stars katika mashindano ya fainali za Kombe la Mataifa ya Africa (Afcon) 2019 nchini Misri. Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo. Wengine ni pamoja na Mkuu wa huduma ya rejareja wa benki ya Exim, Bw. Andrew Lyimo (katikati)
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim, Stanley Kafu (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kampeni maalum inayofahamika kama 'Afconika na Exim' ambayo inatoa fursa kwa wateja wa benki hiyo kulipiwa gharama zote za safari na malazi ili waweze kushuhudia mechi za timu ya taifa, Taifa Stars katika mashindano ya fainali za Kombe la Mataifa ya Africa (Afcon) 2019 nchini Misri. Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo. Wengine ni pamoja na Mkuu wa Hazina na Masoko ya Fedha wa benki hiyo Bw Arafat Haji (Kulia) na Mkuu wa huduma ya rejareja wa benki ya Exim, Bw. Andrew Lyimo (kushoto)
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Exim makao makuu jijini Dares Salaam wakionesha ishara ya ushangiliaji wakati wa uzinduzi wa kampeni maalum inayofahamika kama 'Afconika na Exim' ambayo inatoa fursa kwa wateja wa benki hiyo kulipiwa gharama zote za safari na malazi ili waweze kushuhudia mechi za timu ya taifa, Taifa Stars katika mashindano ya fainali za Kombe la Mataifa ya Africa (Afcon) 2019 nchini Misri. Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...