Na Moshy Kiyungi,Dar es Salaam.

Tupac Shakur alikuwa mwanamuziki maarufu wa muziki wa hip hop kutoka nchini Marekani.

Alifahamika zaidi kwa jina lake la kisanii la 2Pac.

Shakur aliuawa kwa kupigwa risasi Septemba 13,1996 wakati akiwa anaendesha gari mjini Las Vegas, Nevada nchini Marekani.

Alikuwa mmoja kati ya wasanii wa muziki wa Hip hop, waliouza rekodi nyingi za muziki duniani.2Pac alikuwa mtoto wa Afeni Shakur, ambaye alikuwa mwanachama wa Black Panther Party. Mama yake alitolewa jela mwezi mmoja kabla ya kujifungua mtoto wake Tupac.

Shakur alikuwa na vipaji vingi vilivyo vilivyomuongezea umaarufu akiwa na umri mdogo.Vipaji hivyo vya Shakur ni kwamba alikuwa rappa, mwigizaji, mtayarishaji wa rekodi, mshairi, mwanaharakati na mtunzi wa nyimbo. 

Majina yake halisi alikuwa akiitwa ‘Tupac Amaru Shakur’. Maana halisi ya jina Tupac ni Nyoka inayong’ara. Majina ya ‘TuPac Amaru Shakur’ ni makubwa yaliyoweka historia kubwa katika dunia hasa kwenye suala zima la mziki wa Hip-Hop.

Alizaliwa mnamo mwaka Juni 16, 1971 katika jiji la New York, nchini Marekani.Mara nyingi aliitwa 2Pac, Pac, Makaveli na pia mwenyewe akajiita The Don Kiluminati.Tupac, pia alishawahi kushikilia rekodi ya Guinness ya ulimwengu (Guinnes World Record), kwa kuwa na mauzo ya juu sana kwa msanii wa muziki wa rap ya hip hop.

Shakur aliwahi kupata mauzo takriban milioni 74 kwa hesabu ya dunia nzima na milioni 44 kwa mauzo ya Marekani pekee.Alishirikiana na baadhi ya vikundi na wanamuziki wakubwa nchini mwake kama Outlawz, Thug Life, Danny Boy, Digital Underground, Dr. Dre, Johnny "J",Ice Cube, Nate Dogg, The Notorious B.I.G. na Snoop Dogg.

Chanzo cha kifo chake kilielezwa kwamba mnamo Septemba 07, 1996 Tupac alikwenda katika jiji la Las Vegas, kwa ajili ya kuhudhuria pambano la ngumi kati ya bondia Mike Tyson alipokuwa akinyukana na mpinzani wake Bruce Seldon.

Kwa mujibu wa taarifa zilieleza kwamba 2pac alifikia katika hoteli moja ya kifahari jijini Las Vegas iliyokuwa inaitwa Luxor Hotel - Casino.Mpambano huo wa ngumi ulikuwa unafanyiika katika ukumbi maarufu ujulikanao kama MGM Grand Hotel.

Ilielezwa kwamba siku ya mpambano huo, Tupac alihudhuria sambamba na Goons (kampani) yake akiongozwa na Marion ‘Suge’ Knight, ambaye alikuwa mwanzilishi na mmiliki wa record label ya Death Row.Kampuni hiyo ilikuwa ikisimamia kazi za muziki za Tupac ikiwemo kurekodi nyimbo na kadhalika.

Katika mpambano huo, Tupac aliketi kiti kimoja na mlinzi wake aliyekuwa akiitwa Frank Alexander na rafiki wa Suge knight, sambamba na mcheza filamu maarufu wa Hollywood Louis Gossett Jnr.

Wengine waliokuwa karibu naye walikuwa Mchungaji Jesse Jackson, Charlie Sheen pamoja na mchezaji wa baseball aliyevuma wakati huo Reggie Jackson katika eneo la wageni maalumu (V.I.P).

Kwenye pambano hilo kiti kimoja cha V.I.P, kilitozwa kiasi cha dola za kimarekani 1,000, hiyo ilitokana na ukubwa wa pambano hilo.Hivyo watu walioweza kuketi viti vya V.I.P.walikuwa ni mashuhuri na wenye ‘mkwanja’ wa nguvu.

Wimbo alioingia nao Mike Tyson kabla ya pambano lake kuanza, uliandikwa na Tupac Shakur uliokuwa unaitwa ‘Wrote The Glory’.Katika pambano hilo Mike Tyson aliweza kuibuka kidedea baada ya kumchakaza mpinzani wake Bruce Seldon katika raundi ya pili ya pambano hilo.

Baada ya Pambano hilo kuisha, kundi ambalo lilikuwa linaongozwa na Tupac Shakur, liliingia katika mzozo katika sebure ya ukumbi wa MMG baada ya kurushiana maneno dhidi kundi lingine.Chanzo ugomvi huo hakikuweza kujulikana mara moja licha ya kwamba askari wa usalama ukumbini hapo waliweza kuingilia kati ili kuweka hali ya amani.

Ilielezwa kwamba Tupac na kundi lake waliondoka katika eneo hilo la tukio na kuelekea katika Hotel waliyofikia.Kifo hicho kiliacha maswali mengi na simanzi miongoni mwa wapenzi na mashabiki wa muziki kutoka katika kila pembe za dunia.

2Pac Shakur wakati wa uhai wake alikuwa mmoja kati ya marapa waliojizolea umaarufu mkubwa na mafanikio kupitia kazi ya muziki kwenye miaka ya 1990.

Hata hivyo alikuwa na kipaji kingine cha uigizaji.

Septemba 13, 2019, ‘TuPac Amaru Shakur’ atatimiza miaka 23 tangu kutokea kifo chake baada ya kupigwa risasi mnamo Septemba 13,1996 wakati akiwa anaendesha gari mjini Las Vegas, Nevada.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...