Anaandika Abdullatif Yunus.

Halmashauri ya Wilaya Bukoba ipo mbioni kuanza kutekeleza na kujenga Miundo mbinu ya Kudumu ya mradi mkubwa wa kusambaza Maji katika Chuo kipya cha Ufundi stadi VETA kinachotarajiwa kujengwa katika Kijiji cha Burugo, Kata Nyakato mradi utakaogharimu zaidi ya Milioni 900.

Akizungumza na wanahabari Ofisini kwake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukoba, Murshidi Ngeze ameeleza kuwa Mchakato wa kupata mkandarasi tayari umefikia hatua nzuri baada ya zile taratibu za awali kukamilika ambazo ni pamoja na kutangaza zabuni, na tayari Kamati ya fedha imejadili na hivi karibuni itamtangaza Mkandarasi ambae baada ya kutiliana saini ataanza kusambaza kazi ya Ujenzi wa mradi wa Maji katika Chuo hicho, ambapo pia utavinufaisha Vijiji jirani vinavyopakana hapo.

Awali Halmashauri ya Bukoba ilipeleka mradi wa Maji ya awali ya kuanzia yaliyogharimu zaidi ya Milioni 19, ambapo fedha hizo zilitokana na mapato ya Ndani.

Ujenzi wa mradi huu utashirikisha pia wakazi wa eneo husika katika maana ya (Force Account), hivyo wakazi wa eneo hilo watahusishwa katika kazi ndogondogo.

Katika hatua nyingine Ngeze amepokea Vitabu vya ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ambapo kwa miaka mitatu mfululizo sasa Halmashauri hiyo imekuwa ikiibuka na Hati safi, hii ni kutokana na usimamizi mzuri wa sheria katika Halmashauri zinahusu mambo yote ya Kiutawala pamoja na Usimamizi wa mipango yote inayohusu fedha.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukoba Murshidi Ngeze akionesha kwa Wanahabari Vitabu vya Ripoti ya CAG, ikiwa ni Mara ya Tatu mfululizo kwa Halmashauri hiyo kupokea Hati safi wakati akizungumza na Vyombo vya Habari Ofisini kwake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...