Vigogo wa Serie A Juventus wameimiliki Coppa Italia kwa miaka kadhaa ya hivi karibuni na wameshinda mara nne mfululizo hadi msimu uliopita. Lakini baada ya kutolewa na Atalanta kwenye robo fainali, jambo moja liko wazi: Jina la Juventus halitaandikwa kwenye Kombe la Coppa Italia baada ya mchezo wa fainali Mei 15.

Usiku wa leo na kesho michezo ya pili ya nusu fainali itapigwa, timu zote zina nafasi baada ya michezo ya kwanza yote kuisha kwa sare. Lazio mara ya mwisho wameshinda taji hilo mwaka 2013, katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali walilazimishwa suluhu nyumbani dhidi ya AC Milan. Klabu hiyo ya jijini Rome imekuwa na matokeo dhaifu hata kwenye ligi msimu huu, na pengine Coppa Italia ndiyo tiketi yao ya kushiriki kwenye mashindano ya Ulaya msimu ujao.

Lakini ili kufanikisha hilo wanahitaji kuwafunga Milan walau goli moja usiku wa leo, ambapo wenyeji wao wamekuwa wagumu sana kuruhusu magoli. Golikipa wa timu ya taifa ya Italia Gianluigi Donnarumma na Pepe Reina – ambao wameshirikiana kulinda lango la Milan bado hawajaruhusu bao hata moja kwenye Coppa Italia, hii itawaongezea presha washambuliaji wa Lazio. Pia Lazio wanatakiwa kufikiria namna ya kumzuia mshambuliaji wa AC Milan Krzysztof PiÄ…tek, ambaye anaongoza kwa magoli kwenye shindano hilo akiwa na jumla ya mabao nane hadi sasa.

Kama mashabiki waliotazama mechi ya kwanza ya Lazio na Milan walinyimwa burudani ya magoli basi mchezo wa Fiorentina na Atalanta uliwapa burudani yote, timu hizo zilifungana jumla ya magoli sita. Aisee!! Fiorentina na Atalanta wote wana muda mrefu sana hawajashinda taji hilo, Fiorentina mara ya mwisho wameshinda mwaka 2001 wakati Atalanta wameshinda mara moja tu na ilikuwa mwaka 1963.

Atalanta ambao bado wanagombania nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao watakuwa na mchezo mwingine mwisho wa wiki. Beki wa Atalanta Andrea Masiello, ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa mwezi mzima akiuguza majeraha alisema wataingia katika michezo yote wakitafuta ushindi. “Hatutaki kufanya mahesabu kabla ya mechi, kila mchezo tutauchukulia uzito na umuhimu wake kama ulivyo.

“Ni lazima tuendelee kufanya tulichofanya msimu huu, Tuna imani na utaratibu tuliojitengenezea kwani ndio ambao umetupatia matokeo,” aliwaambia waandishi wa habari.
Mchezo wa AC Milan vs Lazio utapigwa leo saa 3:45 Usiku na ule wa Atalanta vs Fiorentina utapigwa kesho Alhamisi saa 3:45 Usiku, zote zitakuwa MUBASHARA kupitia StarTimes World Football pekee katika kifurushi kilichoboreshwa cha UHURU kwa watumiaji wa Antenna na SMART kwa wateja wanaotumia dish.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...