Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Sara Msafiri amewataka wananchi pamoja na Kampuni zilizojenga katika hifadhi ya barabara kuzingatia sheria na taratibu za wakala wa Barbara nchini TANROADS ili kuepuka usumbufu wa kuvunjiwa na kuisababishia serikali hasara.

Kauili hiyo ya Mkuu wa Wilaya MSAFIRI imekuja baada ya kubaini baadhi ya wawekezaji kujenga kituo cha mafuta katika hifadhi a barabara na kuongeza kuwa serikali imekuwa ikiweka mazingira bora ya uwekezaji ili pande zote mbili ziweze kunufaika.

Akiwa katika ziara ya kukagua vituo vya kuhifadhia na kusambaza mafuta ndani na nje ya nchi vilivyopo Wilayani humo amesema, ameridhishwa na ukarabati wa Tanki la Mafuta la Kampuni ya TAZAMA ambalo linajengwa kwa ushirikiano wa Tanzania na Zambia hivyo linapswa kuendelezwa kutokana na historia yake baina ya nchi hizo mbili.

Kwa upande wake Meneja wa Mkoa wa TAZAMA upande wa Tanzania ABRAHAM SAMWEMA amesema ujuio wa mkuu wa Wilaya utasaidia kutatua migogoro iliyopo kati yao na wananchi wanaovamia eneo la bomba la mafuta huku kaimu mkurugenzi wa jeshi la zimamoto na uokoaji CASTORY WILLA akizitaka Kampuni za mafuta kuwa na vifaa bora vya kuzuia milipuko ya moto katika maeneo ya kazi

Ziara hiyo ya siku nne ya Mkuu wa Wilaya wa Kigamboni inahitimishwa Ijumaa kwakuzikutanisha Kampuni za Mafuta na Gesi zilizopo katika wilaya hiyo.
Meneja wa Uhandisi TAZAMA Mhandisi Patrick Mnzava (kulia) akimwelezea Mkuu wa wilaya ya Kigamboni,Sara Msafiri mtambo kusafirisha mafuta ghafi kwenda Zambia unavyo fanya kazi leo katika ziara ya kukagua vituo vya kuhifadhi mafuta leo jijini Dar es Salaam. 
Meneja wa Uhandisi TAZAMA Mhandisi Patrick Mnzava (alienyosha mkono) akifafanua jambo mbele ya Mkuu wa wilaya ya Kigamboni,Sara Msafiri katika ziara ya kukagua vituo vya kuhifadhi mafuta leo jijini Dar es Salaam. 
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni,Sara Msafiri akiwa ameongozana na kamati ya ulinzi ya wilaya hiyo wakikagua mitambo mbalimbali ya kampuni ya mafuta ya TAZAMA katika ziara ya kukagua vituo vyakuhifadhi mafuta leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
picha ya pamoja.

Mkuu wa wilaya ya Kigamboni,Sara Msafiri wa (kwanza kushoto) akizungumza na wafanyakazi wa kampuni ya mafuta ya TAZAMA katika ziara ya kukagua vituo vya kuhifadhi mafuta leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...