Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MKUU
wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar as Salaam Daniel Chongolo amezindua
kampeni maalum ya kuhamasisha wananchi wa wilaya hiyo kulipa kwa wakat
kodi ya majengo pamoja na kodi ya mabango.
Kampeni
hiyo itakwenda sambamba na kampeni ya nyumba kwa nyumba kwa lengo la
kuhakikisha wamiliki wote wa majenga wanalipa kodi kwa wakati na lengo
la Wilaya ya Kinondoni ni kukusanya Sh.bilioni saba katika majengo.
Akizungumza
na Michuzi Blog jijini Dar as Salaam wakati wa kuzindua kampeni hiyo
kwa Wilaya ya Kinondoni iliyofanyika Bunju, Chongolo amesema lengo la
kuzinduliwa kampeni hiyo ni kuhamasisha wananchi kuanza kulipa kodi ya
majengo na mabango mapema.
Ameongeza
kuna tabia ya wananchi wengi kujitokeza siku ya mwisho katika kulipa
kodi ya majengo kiasi cha kusababisha msongamano mkubwa wa watu,hivyo
Wilaya ya Kinondoni imeona ni vema ikaanza kampeni hiyo ili wananchi
waanze kulipa kuanzia sasa na mwisho ni Juni 30,2019.
Chongolo
amesema katika kufanikisha kampeni hiyo viongozi wa ngazi mbalimbali wa
Wilaya wakiwamo watendaji wa mitaa na kata watashirikiana na.maofisa wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kwenda kufanya hamasa hiyo kwa wananchi
na kubwa zaidi kutambua umuhimu wa kulipa kodi ya majengo na mabango.
"Kutakuwa
na utaratibu maalumu wa kila mwenye jengo kupewa stakabadhi inayoonesha
kodi anayostahili kulipa na kisha atakwenda kulipa na watendaji
watakuwa wakiwaelekeza wananchi pakwenda kulipa kodi yao.
"Serikali
kwa kuwajali wananchi wake imeamua kodi ya jengo kuwa moja tu iwe ni
Sh.10,000 tu.Hivyo mwenye nyumba moja atalipa kiasi hicho na mwenye
nyumba mbili atalipia kila nyumba kwa Sh. 10,0000.
"Kwa
wenge ghorofa kila floo italipiwa sh.50,000.Makadirio yetu na matarajio
ambayo tumejiwekea ni kukusanya Sh.bilioni saba kutoka kwenye
majengo.Kampeni hii ambayo tumeizundua tunaomba wananchi washiriki
kikamilifu ili kufikia malengo ambayo Wilaya ya Kinondoni tumejiwekea,"
amesema Chongolo.
Hata
hivyo amesema baada ya kampeni ya kuhamasisha ulipaji wa kodi ya
majengo,yeye mwenyewe kwa kushirikiana na viongozi wa Kara,mitaa na
maofisa wa TRA watakwenda nyumba hadi nyumba kuangalia nani amelipa na
na hajalipa kodi.Hivyo amesema cha msingi wananchi kulipa ndani ya muda
uliowekwa.
Kwa upande
wake Meneja wa TRA Wilaya ya Kinondoni jijini Dar as Salaam Masawa
Masatu amesema wamejipanga kuhakikisha kampeni hiyo inafanikiwa na
watafanya hamasa maeneo yote ndani ya Wilaya huku akifafanua changamoto
ya wananchi kusubiri tarehe za mwishoni wanataka kuiondoa.
"Kuna
tabia ya baadhi ya wananchi ambao wao wanasubiri tarehe ya mwisho ndio
wanakwenda kulipa kodi ya majengo.Kinondoni tunasema watu walipe kodi
ndani ya muda uliopo kwani itaondoa msongamano kwenye maeneo ya kulipia
kodi.Katika majengo tunakadiria kukusanya Sh.bilioni saba," amesema
Masatu.
Wakati huo huo
Mtendaji wa Kara ya Bunju Ibrahim Mabewa amesema kuwa jukumu lao ni
kushiriki kikamilifu kuhakikisha hamasa ya wananchi kulipa kodi inafika
kwenye.mitaa yote na hatimaye kodi ikusanywe kwa ajili ya maendeleo ya
Watanzania wote.
Naye
Msanii maarufu nchini Mrisho Mpoto a.k.a Mjomba ambaye naye alishiriki
kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo amesema wasanii wanalojukumu la
kuhamasisha ulipaji wa kodi na kufafanua tena wanapaswa kuhamasisha kwa
lugha rahisi ambayo itafanya mwananchi alipe kodi.
Amesema
suala la kodi hata huko miaka ya nyuma inaelezwa namna lilivyokuwa
ugumu maana unapozungumzia kodi unazungumzia fedha,hivyo kazi ya wasanii
ni kutoa lugha rahisi lakini yenye kuzungumzia umuhimu ya wananchi
kulipa kodi.
WASANII wa kundi la ngoma za asili linaloongozwa na msanii nyota Mrisho Mpoto, wakitoa burudani kwa kutumia nyoka aina ya chatu, Barabara ya Bagamoyo eneo la Bunju A, ikiwa ni kuhamasisha wananchi kulipa kodi ya nyumba na mabango, wakati wa uzinduzi wa wiki ya ulipaji kodi hiyo, Wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, jana.(Picha na Christopher Lissa).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...