Na Woinde Shizza Globu ya jamii

Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro kwa kushirikiana na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Meru Wametoa ng'ombe 20 kwa watu waishio katika mazingira magumu.

Wakikabidhi ng'ombe hizo Askofu wa dayosisi hiyo Elias Kitoipamoja na mkuu wa wilaya hiyo Jerry Muro wamesema Kanisa pamoja na Serikali wanashirikianapamoja na wadau wa maendeleo katika kuhakikisha wanasaidia wananchi kiroho na kimwili katika kuleta maendeleo yanayolenga kuwaondolea umasikini wananchi.
"Fedha za kununua Ng'ombe hizi zilipatakana kwa shida sana kutoka kwa wadau walioko Marekani , kufuatia mahusiano mazuri kati ya kanisa , serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo ya utoaji wa ng'ombe 20 wenye thamani ya zaidi ya milioni 20 alisema

Askofu Kitoi Alisema kama dayosisi ya Meru hawakuliangalia jambo hilo kibinadamu zaidi walimuomba Mungu ili waweze kufikisha mradi huo sehemu husika ambapo walishirikiana na wakuu wa majimbo, wachungaji pamoja na wainjilisti ili kuwapata wale wahitaji katika sharika zao jambo alilosema limefanyika kwa uaminifu.

Aliongeza kwa kuwataka waliopewa ng'ombe hizo kuwa mawakili wema ili kuwasaidia na wahitaji wengine pindi zinapozaliana huku akisema kuwa wamepatiwa bure bila malipo yoyote isipokuwa katika kila uzao wa kwanza kwa kila ng'ombe atapelekwa Kanisani.

"Tunatamani muendeleze mradi huu ili wengine wanufaike tumeweka utaratibu kuwa kila Mzaliwa wa kwanza wa ndama jike atapelekwa Kanisani ili apatiwe muhitaji mwingine lakini mzaliwa wa kwanza dume ataletwa kanisani kama Limbuko na hii itakuwa manufaa kwa usharika husika"alisema Askofu.

katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Cornel Muro alisema anatambua mchango mkubwa wa Kanisa katika wananchi wa Arumeru ambapo hapo awali walishakabidhi mbuzi kwa wananchi hao

Aidha Muro aliwataka wanufaika wa mradi huo kutumia fursa hiyo kikamilifu lengo likiwa ni kutokomeza umaskini katika Jamii ambapo alisema yeyote atakayeshindwa kutunza ng'ombe hao ni vema akarudisha Katika Usharika wake ili apatiwe mtu mwingine ambaye ni muhitaji .

"Nitoe rai kwa wote mliopatiwa zawadi hii kama mkishindwa kuwatunza ng'ombe hawa warudisheni Kanisani ili wapatiwe wengine wenye uhitaji zaidi na watakaothamini hili"Alisema Muro

Mkuu huyo wa Wilaya aliahidi kutoa ufadhili wa kuchanja ng'ombe wote kama mchango wake na kuunga mkono juhudi za Dayosisi hiyo ambapo alisema pia atawaunganisha na Afisa mifugo wa Halmashauri ya Meruili ng'ombe hao wapatiwe huduma stahiki.

Picha ikionyesha Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akishirikiana na mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Meru Elias katoi wakitoa ng'ombe 20 kwa familia zisizojiweza. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...