Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.

MKURUGENZI  wa Mashitaka Nchini (DPP), ameipa mamlaka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  kusikiliza kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili Yusuf Ali maarufu kama ‘Mpemba wa Magufuli' na wenzake watano.

Hatua hiyo imekuja leo Aprili 25, 2019 kufuatia wakili wa serikali Eliya Athamasi akisaidiana na Candid Nasua ,kuwasilisha hati na ridhaa ya kuruhusu Mahakama hiyo kusikiliza kesi hiyo iliyowasilishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Baada ya kuwasilishwa kwa nyaraka hizo,upande  wa mashitaka uliwasomea upya washitakiwa hao mashitaka yao ambayo waliyakana na upande wa mashitaka umeomba  tarehe ya kuwasomea washitakiwa hao Maelezo ya awali na kesi hiyi imeahirishwa hadi Mei 7 mwaka huu.

Yusuf na wenzake watano, wanakabiliwa na mashitaka manne, likiwemo la kujihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Charles Mrutu, Benedict Kungwa, Jumanne Chuma, Ahmed  Nyagongo  na Pius Kulangwa.

Katika hati ya mashtaka imedaiwaaiwa kwamba Kati ya Januari 2014 na Oktoba 2016  katika Mkoa wa Dar es Salaam, Ilinga, Morogoro, Tanga na Mtwara kwa dhamira,waliendesha na kujihusisha na shughuli za kihalifu kwa kupokea,kumiliki na kujihusisha na biashara haramu ya vipande 50 vya meno ya Tembo vyenye thamani ya Sh. 392, 870,000 bila kibali kutoka kwa mkurugenzi wa Wanyamapori.

Washitakiwa hao pia wanadaiwa kwamba,Oktoba 26 mwaka 2016 eneo la Mbagara Zakiem,Temeke Dar es Salaam walikutwa wakimiliki vipande 10 vya meno ya tembo vyenye thamani ya Sh. 60,496,000 bila kuwa na kibali.

Imeendelea kudaiwa kuwa, Oktoba 27 2016 huko Tabata Kisukuru, wastihakiwa hao walikutwa  wakimiliki vipande vinne vya meno ya tembo vyenye thamani ya sh 32,734,800 kinyume cha shehria. Pia washtakiwa hao wanadaiwa Oktoba 29, walikutwa wakimiliki vipande 36 vya meno ya Tembo  vyenye thamani ya Sh. 294,613,000 bila kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa wanyama pori nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...