Na Woinde Shizza Michuzi TV , Arusha 

Watanzania wametakiwa kudumisha amani na upendo uliopo katika nchi yetu kwani ndio zawadi pekee tulioachiwa na mwenyezi mungu.

Hayo yamebainishwa na nabii mkuu Wa kanisa la Ngurumo ya upako Dr Geordave Kisambale jijini hapa wakati akiongea na waumini Wa kanisa hilo katika ibada ya Chuo cha unabii iliofanyika kosongo jiji hapa. 

Alisema kuwa watanzania tunayo amani ambayo tumezawadiwa na mungu ivyo niwajibu Wa kila MTU kuienzi ,kuidumisha pamoja na kuilinda.

"Unajua mungu anatupendelea sana Watanzania ametupa amani ya nchi yetu ,ametufanya tunaishi kwa upendo angalieni nchi zingine wanapigana kila siku ,kuna vita ndugu kwa ndugu hawapendani lakini sisi watanzania tunaishi kwa amani hivyo ni vyema amani hii tuliopewa tuilinde kama vile mboni ya jicho letu" alisema Geodave

Aidha aliwataka watanzania kutoruhusu mtu yeyote yule kuingilia amani yetu na kuivuruga kwani hii ni zawadi ya pekee tuliopewa na mwenyenzi mungu.

Pia alimtaka kila Mwananchi kupitia imani yake kuendelea kuombea nchi yetu ya Tanzania iendelee kuwa na amani pia aliwakumbusha kuwaeka viongozi wetu Wa kitaifa akiwepo Rais Wa Jamuhuri ya Muungano Wa Tanzania katika maombi kila siku ili mungu aendelee kuwaongoza na kuwapigania.

Aidha amewataka watanzania kutii Sheria za nchi bila vurugu, huku akisisitiza wanasiasa kutopandikiza Chuki miongoni mwa wananchi badala yake wawaunganishe na kuwafanya kitu kimoja.
Nabii Dr Geodave kisambale akihudumia waumini wake .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...