Mkurugenzi wa Maendeleo ya michezo Dk.omar singo akikabidhi mpira kwa mchezaji wa zamani ya timu ya taifa stars ikiwa ni ishara ya uhamasishaji kuelekea michuano ya kombe la afcon pamoja na Mkurugenzi wa masoko wa Kampuni ya multichoice nchini Baraka shelukindo na wafanyakazi wengine wakati wa kutambulisha rasmi kurushwa mubashara kwa michuano hiyo kupitia king'amuzi cha dstv.

  * Kiemba awataka watanzania kuwa wazalendo kuwatia moyo wachezaji
     
      Na.Khadija seif,Globu ya jamii

WATANZANIA wametakiwa kuwa wazalendo kwa vitendo na kuonyesha umoja na mshikamano  katika kuelekea michuano ya kombe la AFCON ya hivi karibuni.

Akizungumza katika hafla ya kuzindua kampeni hiyo ya DStv ijulikanayo kama ‘DStv Inogile’, Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania Ronald Baraka Shelukindo amesema kuwa katika kuunga mkono kampeni ya kuifanya nchi yetu ifanye vizuri katika michezo mbalimbali, DStv imehakikisha kuwa michuano mbalimbali ya kimataifa inarushwa mubashara .

"Kupitia  kifurushi cha chini kabisa cha DStv Bomba cha Sh. 19,000 tu hivyo kuwawezesha mamilioni ya watanzania kuziona timu zetu na hivyo kuongeza ari ya kuziunga mkono kwa hali na mali," alisema shelukindo.

 Huku mkurugenzi wa Maendeleo ya michezo Dk. Omar singo amesema ni wakati wa kushangilia kufa na kupona vijana wa chini ya miaka 17 ambao wamefuzu kuingia katika michuano hiyo .

Pia amewapongeza kampuni ya multichoice nchini kupitia king'amuzi cha dstv kwa kuendelea kutoa mchango mkubwa katika sekta ya michezo.

"Serikali inathamini sana michango ya aina mbalimbali inayotolewa na wadau kama hao katika kukuza michezo na kuimarisha michezo hapa nchini", alisema singo.

Kwa upande wake mchezaji nguli aliewahi kuichezea timu ya taifa Edibily lunyamila amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi uwanjani ili kuwapa hamasha na morari wachezaji wetu wa Serengeti boy wenye umri chini ya miaka 17 .

"Kwa mara ya Kwanza Tanzania imepewa heshima kubwa ya kuandaa mashindano haya makubwa hivyo ni wakati wetu sisi watanzania kuonyesha uzalendo ," alisema lunyamila.

Hata hivyo ametoa rai kwa watanzania kujitokeza uwanjani kuwatia moyo vijana ,ili kuhakikisha wanashinda katika michuano hii na kupata tiketi ya kwenda kwenye mashindano ya dunia nchini Brazil .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...