Mwenyekiti wa Halmashuri ya wilaya ya Iringa, Stephen Mhapa akikabidhiwa funguo za gari aina ya Toyota Hiece na mwakilishi wa IBO Iringa DC, Paola Ghezzi alisema kuwa shirika lisilo la kiserikali la IBO limekuwa likijishughulisha na elimu maalumu kwa kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalumu,watoto wenye mazingira magumu na watoto wenye ulemavu. Mwenyekiti wa Halmashuri ya wilaya ya Iringa, Stephen Mhapa akiwa kwenye gari hilo aina ya Toyota Hiece baada ya kukabidhiwa na shirika lisilo la kiserikali la IBO lililoko nchini Italy kwa ufandhili wa wadau kama Waldesian Church,Emilia-romagna Region,Ferrara Town,Helpicare na Nyumba ya Ali
Gari aina ya Toyota Hiece lilokabidhiwa na shirika lisilo la kiserikali la IBO lililoko nchini Italy kwa ufandhili wa wadau kama Waldesian Church,Emilia-romagna Region,Ferrara Town,Helpicare na Nyumba ya Ali
Baadhi ya wafanyakazi wa Halmashauri ya Iringa wakifurahia kupokea kwa msaada wa Gari hilo




NA FREDY MGUNDA, IRINGA.

HALMASHAURI ya wilaya ya Iringa imepokea msaada wa gari aina ya Toyota Hiece kwa ajili ya wanafunzi wa elimu maalumu katika shule ya msingi Kipera kutoka kwa shirika lisilo la kiserikali la IBO lililoko nchini Italy kwa ufandhili wa wadau kama Waldesian Church,Emilia-romagna Region,Ferrara Town,Helpicare na Nyumba ya Ali.

Akizungumza wakati wa kukabidhi Gari hilo mwakilishi wa IBO Iringa DC, Paola Ghezzi alisema kuwa shirika lisilo la kiserikali la IBO limekuwa likijishughulisha na elimu maalumu kwa kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalumu,watoto wenye mazingira magumu na watoto wenye ulemavu.

“Shirika hili linafanya kazi na halmashuri ya Iringa kwa kusaidia watoto wenye changamoto hizo hapo juu kwa lengo la kuwasaidia kiuchumi na kuwawezesha kupata mahitaji yao kama ilivyo kwa watoto wengine wanaopata mahitaji yote muhimu” alisema Ghezzi

Ghezzi alisema kuwa shirka hilo tayari limeshasaidia ujenzi wa jiko la shule ya msingi Kipera yenye watoto mchanganyiko na watoto wenye ulemavu na ujenzi huo bado unaendelea katika shule hiyo kwa lengo la kutoa hudumu bora kwa wanafunzi wa shule hiyo.

“Tumefanikiwa kujenga Ramps katika shule nne za halmashauri ya Iringa ambazo ni Ismani,Idodi,Ihehelo na Tungamalenga kwa lengo la kuwasaidia watoto wenye ulemavu kupita bila kupata usumbufu wowote ule” alisema Ghezzi

Aidha Ghezzi alisema kuwa shirika hilo limefanikiwa kutoa mafunzo kwa walimu zaidi ya arobaini (40) kwa kuwaongezea maarifa kwa ajili ya kufundisha elimu maalumu kwa wanafunzi wanahitaji elimu hiyo katika halmashauri ya Iringa katika kata za Idodi na Ismani tayari washapewa mafunzo.

“Tumefanikiwa kutoa semina na maonesho kwa jamii juu ya umuhimu wa elimu maalumu kwa kata ya Ismani ambapo shirika limefanikiwa kutoa elimu hiyo kwa jamii hadi hivi sasa” alisema Ghezzi

Akipokea gari hilo aina ya Toyota Hiece mwenyekiti wa halmashuri ya wilaya ya Iringa, Stephen Mhapa aliwakikishia shirika la IBO kuwa msaada ambao wamekuwa wakiutoa katika halmashauri hiyo utatumika kama ulivyokusudiwa na miradi yote itatunzwa kikamilifu.

“Mmetusaidia sana miradi mingi hivyo sisi tunaahidi kutunza na kuthamini miradi na uwepo wenu katika halmashauri hii ambapo mmetusaidia kuwaokoa watoto wenye mahitaji maalumu,watoto wenye mazingira magumu na watoto wenye ulemavu” alisema Mhapa

Mhapa alisema kuwa imekuwa vigumu mno kumlea mtoto mwenye mahitaji maalumu,mtoto mwenye mazingira magumu na mtoto mwenye ulemavu kwa kuwa inahitaji uangalizi mkubwa mno ila shirika la IBO limetusaidia kulea watoto hao.

“Namna ilivyo tabu kumlea mtoto mwenye mahitaji maalumu,mtoto mwenye mazingira magumu na mtoto mwenye ulemavu,wakina mama mnajua ilivyo kuwa kazi ngumu hivyo tunaomba kutoa shukrani zetu kwa wadau ambao wanatusaidia kulea watoto hao” alisema Mhapa

Mhapa alimalizia kwa kuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya Iringa kuhakikisha wanawaandikia barua ya shukrani kwa shirika la IBO kwa kuasiadia miradi mbali mbali ambayo imekuwa ikiwasaidia watoto wenye mahitaji maalumu,watoto wenye mazingira magumu na watoto wenye ulemavu.

Lakini Mhapa aliomba shirika hilo kuendelea kuwasaidia katika mahitaji mbalimbali kwa kuwa bado halmashauri hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi za watoto hao na nyingi zinazoshabiana na changamoto hizo hivyo mkipata kitu tunaomba mtukumbuke ili tuendelee kutatua changamoto hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...