Na Moshy Kiyungi
Bendi ya Tabora Jazz ilikuwa na makazi yake mjini Tabora ikipiga muziki wake katika ukumbi wa nyumbani wa Lumumba. Ilikuwa na sifa ya kutoka na nyimbo mpya kila baada ya kipindi fulani, ambazo zotezilikuwa zikiwagusa baadhi ya watu. Wakati huo nyimbo za bendi hiyo zilipigwa mno kwenye kumbi za starehe pamoja na kituo cha Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) na vituo vingine vya Radio vya Afrika ya mashariki.

Bendi hiyo ilitamba kwa mitindo yake ya za Segere Matata, Segua Segua na Mambo mileka. Mji wa Tabora unaelezwa kwamba ulianza kupata burudani za muziki wa dansi hata kabla ya chama cha TANU hakijaanzishwa.

Mwandishi wa makala hii alimtembelea mzee Hassan Athumani, aliyewahi kuwa mwanamuziki akipiga gitaa la solo katika bendi za Tabora Jazz, Kiko Kids, Nyanyembe Jazz na Milambo Jazz ‘Sona Sona’ kwa nyakati tofauti. Hassan alisimulia kuwa mnamo mwaka 1953, ilianzishwa bendi ya muziki wa dansi iliyopewa majina ya Staff Jazz, ikiongozwa na Hamisi Wampa.
Vyombo vya muziki vya bendi hiyo vilinunuliwa na mfadhili mmoja wa kabila la Kimmanda’ toka nchini Malawi, wakati huo akiwa ni mfanyakazi wa Bomani.

Staff Jazz ilikuwa na mdhamini akiitwa mwalimu Hasanari. Waanzilishi wa bendi hiyo kati ya miaka ya 1953 hadi 1958, walikuwa akina Hamisi Ali Songo aliyekuwa akipiga ngoma kubwa, Hamisi Ngege alikuwa mpiga ngoma ndogo, Dani Kafumu na Nzige aliyekuwa akipulizaji tarumbeta.

Wengine ni Akbaru Hasanari Dremsi alikuwa akipiga ngoma kubwa, Joseph Kayombo ‘Bambo’ alikuwa mwimbaji, Moshi akichanganya marakasi, Saidi akizidunda ngoma ndogo, Haji Sungura mlinda mlango, Swedi Mandanda na Hamisi Issa wakipuliza tarumbeta na rhythm.

Wanamuziki wengine walikuwa akina Abdi Fundi upande wa saxophone, Athuman Tembo aliyekuwa mwimbaji na kucharaza gitaa la solo, Zakaria Tendawema na Sylvester Chifunda walikuwa waimbaji. Wengine ni Juma Athumani ‘Juma Lumango’ aliyekuwa akichanganya drums na Mlekwa Suleimani mmoja wa viongozi na Rajabu Risasi upande wa gita la besi.

Bendi ya Staff Jazz ilikuwa ikipiga muziki kwenye ukumbi wa baa ya Rufita, ambao baadae ukabadilishwa jina kuwa Lumumba, uliokuwa katika kona ya barabara za Rufita na Kapembe, katikati ya mji wa Tabora. Kwa sababu ambazo hazikuainishwa bendi hiyo kwa mwaka 1954 ilisambaratika.

Busara na hekima za Hamis Alli Songo zilimfanya aifufue bendi hiyo mwaka 1956 kwa jina lingine la Tabora Jazz. Yaelezwa kuwa Mlekwa Selemani aliyekuwa shabiki mkubwa wa bendi ya Kiko Kids, alijiunga na Tabora Jazz na kuwa mmoja wa viongozi wa bendi hiyo. Mwaka 1958 bendi hiyo ilichukuliwa kwenda mikoa ya Kanda ya Ziwa, kwa ajili ya kuhamashisha nguvu ya chama cha TANU.
Katika msafara huo waliongozana na viongozi wake Rashid Mfaume Kawawa, Mzee Herman Pacha, Mama Mosi Tambwe na mumuwe Abdallah Selemani Tambwe. Bendi iliporudi Rashidi Hazuruni aliondoka kwenda Dar es Salaam akajiunga na Cuban Branch iliyokuwa ikiongozwa na Mzee Mwaipungu mwaka 1959. Kati ya mwaka 1960 na 1961 bendi ilikuwa na wapigaji gitaa la solo wawili akina Abdi Fundi na Matata. Mwaka uliofuatia Athumani Tembo akaongezeka katika ukung’utaji wa gitaa hilo.

‘Maisha ni kuhangaika’ usemi huu ulijionesha wakati Rashidi Hazuruni aliporejea tena kupiga muziki na Tabora Jazz mwaka 1963. Tabora Jazz ilisheheni wanamuziki wengi wakiwemo akina Hamisi Wampa aliyekuwa Kiongozi, Hamisi Alli Songo na Akbaru Hasanari Dremsi walikuwa wadunda ngoma kubwa, Mambosasa alikuwa akipiga ukulele (gitaa la kizamani).

Mzee Mambosasa ndiye aliyekuwa baba mzazi wa Athumani Mambosasa, aliyewahi kuwa mlinda mlango wa Klabu ya Simba. Said na Hamis Ngege walikuwa wakipiga ngoma ndogo, Dani Kafundu na Nzige walikuwa wapulizaji wa tarumbeta wakati Joseph Kayombo ‘Bambo’ alikuwa mwimbaji.

Kwa upande wa marakasi alikuwemo Moshi, Haji Sungura aliyekuwa mlinzi ‘mlangoni’, Swedi Mandanda alikuwa mcharazaji wa gita la solo, Hamisi Issa alikuwa akipiga gita la kati ‘rhythm’ na Tarumbeta.

Wanamziki wengine walikuwa Athumani Tembo kwenye solo, upande wa gita la rhythm walikuwa Hamis Issa na Hassan Athumani.

Besi liliungurumishwa na Kassim Mponda aliyeondoka katika bendi hiyo mwaka 1965 mwishoni, akifuatana wanamuziki wengine akina Rashidi Hazuruni na Omari Kayanda wakaenda kujiunga na bendi ya Western Jazz ya jijini Dar es Salaam.

Mwaka 1966 Tabora Jazz ikapata mpiga solo mwingine aliyejulikana kwa jina la Stan, akaziba pengo la Rashidi Hanzuruni. Shaddie aliyekuwa Chotara wa Kihindi naye alikuwepo katika safu ya wapiga gita kati ya miaka 1966/1968. Upande wa safu ya waimbaji walikuwa Athumani Tembo, Omari Kayanda , Sylvester Chifundu, Athumani Ngozi na Joseph Kayombo ‘Bambo’ Mpigaji bongos (ngoma ndogo) alikuwa Juma Athumani ‘Kisegeju’ Abdi Fundi alikuwa akipuliza saxophone ‘mdomo wa bata’.

Kwa upande wa upigaji tumba alikuwepo John Kajos Komba ambaye baadae aliondoka nafasi yake ikazibwa na Ally Mbaruku ‘Ally Sanaless’. Kati ya mwaka 1964 na 1965 Tabora Jazz walirekodi nyimbo baadhi yake zikiwa za Ndugu sikilizeni, Tuambie, Dunia haina mwisho, Mwanawanyeje na nyinginezo.

Mwaka 1967 Kassimu Kaluwona alikwenda Kigoma na kuweza kuwaleta wanamuziki akina Wema Abdallah, Hamis Kitambi, Mabrushi Ramadhani Mgoligwa na Hamisi Mkongo. Mwaka 1968 Salumu Luzira akaijunga na Tabora Jazz akitokea Nzega.

Mwaka 1971 Wema Abdallah akaondoka Tabora Jazz akaenda Western Jazz, nafasi yake ikachukuliwa na mpiga solo mwingine aliyejulikana kwa jina la Kalii, alikitokea Kigoma Jazz. Shem Karenga aliletwa na Kassim Kaluwona toka Kigoma, kuja Tabora kujiunga na bendi hiyo Aprili 1972. Pia alikuwepo mpigaji wa gita la solo Issa Ramadhani ‘‘Baba Watoto’

Kwa kipindi kifupi Said Mabera na Hassan Rehani Bichuka nao walijiunga na Tabora Jazz wakitokea Rumonge Jazz. Aidha mwanamuziki Shaaban Dede, alichukuliwa kujiunga na Tabora Jazz, akitokea bendi ya Milambo Jazz ‘Sona Sona’ ya mjini Tabora.

Shem baada ya kutua, alishiriki vilivyo katika utengenezaji wa wimbo wa Dada Asha ambao baadae ukaibwa na bendi ya Sokous Stars, ulikuwa ni utunzi wake Shem Karenga. Wanamuziki wa Soukous Stara ya nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, waliuchakachua wimbo huo ppamoja na wa Vigeregere uliopigwa na Western Jazz.

Tabu Ley aliiona album yenye wimbo huo wa Dada Asha akiwa Nairobi na aliinunua akaenda kuiuza nchini Kongo, Poland na Ubelgiji. Bendi hiyo baadae akajipanga upya kwa kupata damu changa ili kuendeleza muziki wake. Iliongeza watunzi na waimbaji wengi akiwemo Msafiri Horoub, Madaraka Morris, Ismail Wangoko na wengine wengi. Kwa umoja wao wakafyatua nyimbo nyingi zilizoweza kuridhisha nyoyo za wapenzi na mashabiki wa Tabora Jazz.

Nyimbo hizo ni Ashura, Helena, Dada Remi, Mapenzi ulimi, Visa uache, Lucie umeniacha, Zabibu na Niambie leo Kaka. Zingine zilikuwa za Usijifanye Mwewe, Mariam mpenzi, Zabibu No.2, Sofia mpenzi, Tatu, Serafina, Tamaa yako na Asha No. 1. Nguli hao waliachia vibao vingine vilivyoweza kutamba mno wakati huo, Alhamdulilah na Nashukuru sana.

Nyingine ni pamoja na Dada Mwantumu, Ujana una mwisho, mwisho wake ni uzee. Zingine zilikuwa za Salima, Mapenzi Ulimi, Dada Remmy na Rukia wajidanganya.

Wengi wa wanamuziki wanaotajwa katika makala hii wamekwishafariki. Walio hai ni Hassan Athumani, Madaraka Morris, Ismail Wangoko, Ramadhani Mwanangwa waliokuwa wapiga gitaa la rhythm, Salumu Luzira kwa upande wa gitaa la besi, na wengine wengi.

Bendi ya Tabora Jazz haipo tena katika ulimwengu wa muziki, limebaki jengo bovu likionekana katika kona ya barabara za Rufita na Kapembe, katikati ya mji wa Tabora!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. BALAA TUPU!! NCHI ILIKUWA NZURI WAKATI WA MKOLONI!! ILA MTU MWEUSI KUACHIWA NCHI NA MADARAKA DAAH!! NI UKOMA MTUPU! WATU WOOTE NI WAKOMA!! NA WAZEE WOOTE WALIOKUFA NA KUTANGULIA BAADA YA UHURU WALIKUFA KWA UKOMA WA UHURU!! NYERERE MASIKINI YA MUNGU HAKUWA NA UWEO WOWOTE WA KUENDESHA NCHI! MASIKINI ALIKUWA ANABAHATISHA TU NA KUWAFUNGA WAISLAMU NA KUUWA WATU LAKINI MWISHOWE WALAAYAZID DHALIMIIN ILA KHASARA!! YULE KIBUDU KAFIRI MWENYE GOVI KAMA MJOHORO ALIFIRA NCHI IKANUKA NJAA! NA YEYE AKAONA AMRUSHIE MZIGO ALLY HASSAN MWINYI! LAKINI NA HUYO ALLY HASSAN MWINYI HANISI KAIBA SAANA YEYE NA SITIO MWINYI NA LILE TOTO LAKE HASSAN ALLY MWINYI!¬ SEA CLIFF,WHITE SAND,RAHA TOWER,SLIPWAY.MM STEEL.SUBHASH PATEL,SAYONA DRINKS,KIBOKO PAINTS!!!! WALLAH NAAPA MWINYI KAMA HUJARUDISHA HAYO MADHULUMA YOOTE ULIOIBA NA LEO HII UNA MIAKA 92 NA MUDA WOWOTEE UNAKATA ROHO!! HUYO SITI LIZEE LIAJUZA!! NA HILO TOTO LAKO HASAN MWINYI ZEE HAWATOKUSAIDIA WAKATI UDONGO TANI SABA UKIKUFUNIKA!!!!!! ILA AMALI NJEMA TUUUUU!! NA KABURI YAKO ITAKUWA GIA NA KUKUBANA PUMZI LAANATULLAH WEWEEEEEEE!"! NA HUO UALHAJ NDIO UTAKUCHOMA HUKO KAABURINI LAANATULLAH WEWE!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...