Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli imedhamiria kuiwezesha Sekta ya Afya nchini ili kuimarisha huduma ya afya kwa mama na mtoto.

Dkt Godlove Mbwanji ametoa kauli hiyo mara baada ya utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa Jengo la wazazi kitengo cha META uliofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya.

Alisema Mradi huo wa upanuzi kwa kiasi kikubwa utasaidia kuongeza kwa upatikanaji wa huduma za kina mama wajawazito na watoto wachanga na kuwapunguzia akina mama shida ya kufuata huduma hiyo sehem nyingine.

“Ukamilifu wa ujenzi huu itakuwa ni neema kwa akina mama wajawazito wanaohitaji huduma ya uzazi kwa Ukanda huu wa Nyanda za Juu Kusini.

Tunategemea kukamilika kwa jengo hili tutakuwa na ongezeko la vitanda 200, wataalamu na huduma za kisasa, lengo ikiwa ni kumfanya huyu mama kuwa salama na kupunguza idadi ya vifo vya wajawazito na watoto wachanga". Alisema Dkt Mbwanji.

Mradi huu unatarajia kukamilika ndani ya miezi 18 na utakagharimu chini ya shilingi Bilion 8.4 kwa kuwa unateklezwa kwa kutumia mfumo wa Force Account.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda, Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji pamoja na Mhandisi Juma Mvumbo(Kutoka ZM SUMA JKT), katika utiaji saini Mkataba wa ujenzi wa Jengo jipya la gorofa tano Kitengo cha Meta katika Hospitali Rufaa ya kanda, Mbeya. Utiaji saini huo umeshuhudiwa na Viongozi mbalimbali wa Hospitali akiwemo Mhasibu Mkuu wa Hospitali Bi. Proce Gabone wa kwanza kutoka kushoto mbele na Mshauri elekezi Dkt. Duwa Chenguza (kutoka MCB MUST) wa tatu kutoka Kulia mbele.
Mhandisi Bw. Juma Mvumbo kutoka SUMA JKT akimpatia maelezo Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya na viongozi mbalimbali wa Hospitali juu ya Ujenzi wa Jengo la jipya la Mama na mtoto katika Kitengo cha Meta Hospitali ya Rufaa ya Nyanda za Juu Kusini Mbeya baada ya utiaji saini Mkataba wa uanzaji wa ujenzi huo.
Muonekano wa Jengo litakavyokuwa baada ya kumalizika kwa mradi, Matarajio ni ongezeko la utoaji huduma za kulaza vitanda 200, vyumba 2 vya upasuaji mkubwa na chumba maalum cha huduma za watoto wadogo ndani ya mwezi mmoja (Neonatal Intensive Care Unit) katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya linalotarajiwa kugharimu chini ya shilingi bilioni 8.4 litakapokamilika kwa kutumia mfumo wa Force account.
Mkurugenzi Mtendaji Dkt Godlove Mbwanji, Akimkabidhi mkataba wa ujenzi wa mradi wa Jengo la wazazi Kitengo cha META kwa Mhandisi Juma Mvumbo kutoka SUMA JKT. Ujenzi wa Mradi unategemea kuanza hivi karibuni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...