Ijue vema logo ya Tanzania Diaspora 2019 Day inaendana na kauli mbiu ya mwaka husika. Mwaka huu ni "Oldvai Gorge - Where it all Began".

Mtafiti Dr. Leakey aligundua fuvu ambalo lilthibitika kuwa ni la miaka zaidi ya milion moja. Baada ya ugunduzi huo mkewe Dr. Leakey, Mary akiendelea na utafiti kwenye aneo la Leatoli akagundua nyayo ambazo zilithibitika kuwa ni za miaka zaidi ya milioni tatu.

Mwaka huu 2019 mwezi July itakuwa maadhimisho ya miaka 60 tangu ugunduzi huu na imekuwa kheri kwani na kauli yetu Tanzania Day ni ya kuhusiana na ugunduzi huo.

Sasa kuhusu logo. Ukiangalia logo unaona kama mguu na kiatu, lengo ni kusisitiza kuwa tangu wakati wa peku hadi viatu. Na nyayo inaelekea kaskazini kwani hata za Leatoli zilikutwa hivyo na inasadikiwa kuwa watu walitoka kusini kuelekea kaskazini hivyo imani ni kuwa wote ni "Diaspora" kutoka ...jibu unalo tujivunie.

Kwa wale ambao ni wataalam, kuna imani kuwa binadamu au zamadamu walilipoongezeka ukubwa wa ubongo ndiyo maarifa yalipozidi, kufuatia ugunduzi huu wa Oldvai inaaminika kuwa si ukubwa wa ubongo ila walipoanza kutembea wima wakawa na mikono ilikuwa free kufanya vitu vingine hivyo uvumbuzi wa zana ukawezekana.

Basi niishie hapa nadhani nimejibu na kukusisimua juu ya maana ya logo, chimbuko la diaspora na uzuri wa tulikotoka. 

Mungu ibariki Tanzania na watu wake. Karibu Dallas kama hutoweza wafahamishe na wakaribishe wengine wote tusaidiane kubrand our beautiful nation, Tanzania.

Tutakuwa na wageni na pia kuwatambua

Mr. Erasto Mpemba - Google him and also search for "Mpemba Effect" on YouTube 

Bernard Kiwia - mbunifu toka Arusha

Prof. PLO Lumumba toka Kenya

Prof. Yanda Nobel prize winner from Tanzania 

Mr. Joseph Kussaga 

Balozi wa AU

Wewe na wote utakaowaalika wewe

tanzaniaday.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...