Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Morogoro, Francis Heri Hoza akizungumza na kuunga mkono hoja mbalimbali zilizotolewa na jumuiya ya wazazi na wawakilishi wengine katika kuleta mabadiliko ya kimaendeleo mkoa kwa Morogoro na kukipa kipaumbele kilimo cha misitu na ufugaji wa nyuki.
Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Francis Henry hozza pamoja na Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Morogoro Shaka Hamidu Shaka na katibu wa siasa, itikadi na uwenezi mkoa wa Morogoro Anthony Muhando wakisikiliza michango mbalimbali inayotolewa na jumuiya ya wazazi Morogoro.

 *Hozza amesema Morogoro ni mkoa kwa kipekee kwa misitu

Na.Khadija Seif, Globu ya jamii

BARAZA  kuu la wazazi mkoa wa Morogoro limefanyika na kuadhimia kuisaidia jamii kwa kutoa mafunzo ya ufugaji wa nyuki na  kilimo cha mihogo katika mkoa wa Morogoro ili kuchangia ukuaji wa kiuchumi na kuikwamua jamii katika kutokomeza kasi ya umasikini.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kupokea hoja
Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi mkoa wa Morogoro Francis Heri Hozza amesema mkoa wa Morogoro umejaaliwa misitu mingi na ardhi yenye rutuba kwahiyo kama jumuiya inahitajika kutumia fursa hiyo kuanzisha miradi ya kiuchumi kama ufugaji wa nyuki kama zao la biashara lakini pia kama njia ya kuzuia wanyama wasiharibu mazao ya wakulima na kilimo hususani cha mihogo.

Na pia kutoa fursa kwa jamii kujifunza na kuwatafutia masoko ili kushiriki katika kuunga mkono jitihada za mhe Rais katika kutoa fursa za wananchi kujiajiri .

"kazi ya jumuiya ya wazazi sambamba na kufanya shughuli za kisiasa lakini pia ni pamoja na kuisaidia jamii kivitendo kwa kuwajengea uwezo wa kutambua fursa na kuzitumia ," alisema hoza

Hata hivyo hozza ameeleza kuwa  wataalamu wataletwa kutoa mafunzo ya kilimo cha mihogo na ufugaji wa nyuki kwa jumuiya ya wazazi pia wataalikwa wananchi, makampuni, mashirika, vikundi mbalimbali vya ujasiriamali ili viweze kunufaika na mafunzo hayo.

Alikadhalika hozza amefafanua zaidi kuwa mbali ya kutoa mafunzo hayo kwa umoja wa wazazi wilaya zote lakini pia itazialika jumuiya nyingine za chama, makampuni, watu binafsi, vikundi mbalimbali vya ujasiriamali, asasi za kiraia na watu wa makundi maalumu na kadhalika ili kuwapatia fursa hii muhimu ya kupata utaalamu utakaowawezesha kujiajiri.

Kwa upande wake Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Morogoro Shaka Hamidu Shaka ambae amempongeza katibu mkuu wa chama cha mapinduzi (CCM) dk.Bashiru Ally Kwa uchapakazi wake mzuri hususani mkoani Morogoro ambapo mara kwa mara amefika kushughulikia kero mbalimbali za chama na serikali, na kuitaka jumuiya ya wazazi mkoa wa Morogoro kushiriki kikamilifu katika tamasha kubwa la uzinduzi wa kauli mbiu ya Morogoro ya kijani litakalofanyika hivi karibuni.

" Nampongeza  mhe Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa ziara nzuri anazozifanya za kukagua utekelezaji wa ilani ambazo zina matokeo chanya na mafanikio makubwa kwa maslahi ya taifa," alisema Shaka.

Ametoa rai kwa wananchi wa mkoa wa Morogoro kujitokeza kwenye mafunzo ya ujasiliamari pindi wakufunzi watakapowasili .

Nae katibu wa siasa, itikadi na uwenezi mkoa wa Morogoro Anthony Muhando ameipongeza jumuiya ya wazazi mkoa wa Morogoro kwa kufanyakazi vizuri na kuitaka iendelee kusimamia na kuwa mfano wa maadili na malezi ndani ya mkoa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...