Waziri Mkuu wa Mstaafu Mh Mizengo Pinda akisalimiana na wake wa marehemu Sokoine Mara baada ya kuwasili nyumbani kwa hayati Moringe Sokoine Monduli juu kwa ajili ya misa
Waziri Mkuu wa Mstaafu Mh Mizengo Pinda akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili nyumbani kwa hayati moringe Sokoine Monduli juu kwa ajili ya kushiriki misa
Askofu wa mkuu wa jimbo la kuu katoliki mkoani Arusha Isack Aman akiwa analibariki kaburi la hayati waziri mkuu wa zamani Moringe Sokoine
kadinali Polycarp Pengo akiwa anawasili viwanja vya Waziri mkuu wazamani hayati Moringe Sokoine kwa ajili ya kuendesha ibada ya maadhimisho ya miaka 35

Baadhi ya Wageni waalikwa mbalimbali waliofika kushiriki ibada ya maadhimisho ya miaka 35 ya Hayati Moringe Sokoine

Wake wa marehemu Hayati Moringe Sokoine wakiweka kwa pamoja shada la maua katika kaburi la marehemu mume wao



Woinde Shizza Globu ya jamii

WATANZANIA wameshauriwa kutokuwa chimbuko la kuleta mafarakano na uvunjifu wa amani hapa nchini Tanzania badala yake wawe chanzo cha chanzo cha amani kwa taifa letu na dunia kwa ujumla

Ushauri huo umetolewa leo Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo wakati wakati akiongoza ibada ya maadhimisho ya miaka 35 ya kumbukumbu ya Waziri Mkuu wa zamani hayati Edward Moringe Sokoine ambapo Misa imefanyika nyumbani kwake nyumbani kwake Monduli Juu mkoani Arusha.

Amesema ni wajibu wa kila mtanzania kuhakikisha anailinda amani ya nchi yetu na kutokubali kabisa mtu kujaribu kutushawishi kwa njia yote ile kuvuruga amani ambayo iliasisiwa na wazee wetu wa zamani akiwemo Edward Sokoine pamoja na muasisi wa Taifa hili Hayati Julius Nyerere.

Ameongeza kuwa chimbuko la ukosefu wa amani unatokana na ubinafsi wa watu ambao wamepata uwezo lakini wakataka kuendelea kujikusanyia mali hata kama wengine wanakufa na njaa.

Wakati huo huo akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dk.Augustine Mahiga amewataka wananchi kujijengea tabia ya kuwa na nidhamu katika kufanya kazi.

"Unajua hayati Sokoine alikuwa ni mchapakazi ,alikuwa anafanya kazi kwa bidii ,pia alikuwa ni kiongozi alikuwa anajua umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii na pia alikuwa akikupa kazi na usipoifanya vizuri lazima atakupa adhabu hivyo ni muhimu kuyaenzi yale mema yote aliyoyafanya,"amesema Dk.Mahiga.

Kwa upande wake Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda amesema kuwa hayati Sokoine kama mzalendo alihakikisha kuwa wananchi wote wanaishi maisha sawa.Pia alitumia nguvu kubwa kukabiliana na mafisadi pamoja na wahujumu uchumi katika nchi yetu.

Akitoa shukrani kwa wote waliouthuria Misa hiyo mtoto wa hayati Soikoine Balozi Josephy Sokoine amesema kuwa baba yao alikuwa na anatabia ya kusaidia wanyonge pamoja na wale wananchi wasiojiweza, hivyo wao kama familia wameamua kutumia siku hii ya Aprili 12 kwa ajili ya kusaidia wananchi wasiojiweza kwa kutoa kadi za bima ya afya kwa familia 100 ambazo azina uwezo.

Pia amesema wanatarajia kugawa kadi 600 za bima ya afya ambazo wamezitoa bure na kuongeza wametumia siku hii ya leo kutoa dawa kwa ajili ya zahanati ya Monduli Juu ,ambapo alisema kuwa dawa hizo zinathamani ya Sh. milioni 2.3.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...