*Kesho asubuhi kutua nchi kavu, mikoa ya Lindi,Mtwara na Ruvuma yatajwa
*Kasi yake ya upepo yazidi kuongezeka kadri kinavyosogea katika nchini yetu

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii


MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA) imetoa muelekeo wa kimbunga Kenneth ambacho kwa sasa kipo Bahari ya Hindi ambapo hadi asubuhi ya leo kilikuwa tayari kipo katika Pwani ya nchi yetu na Pwani ya Msumbiji na kimeshakuwa na jicho na hivyo kuwa na nguvu kubwa.

Hivyo TMA imeendelea kusisitiza wananchi kusikiliza na kufuata ushauri unaotolewa na Serikali kwa lengo la kuhakikisha athari zitokanazo na kimbunga hicho ikiwemo ya maafa yanapungua huku ikifafanuliwa kimbunga hicho kesho kitatua nchi kavu katika ardhi ya Msumbuji lakini upepo wake utafikia mikoa ya Kusini ya Lindi, Ruvuma na Mtwara.

Akizungumza leo Aprili 25,2019 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dk.Agnnes Kijazi amesema wamefuatilia muelekeo wa kimbunga hicho ambacho kutokana na muelekeo wake kipo pia Visiwa vya Comorro.

"Muelekeo wa kimbunga hiki kwa sasa kipo Bahari ya Hindi na kinaendelea kusogea kuelekea maeneo ya nchi yetu na mpaka kufika leo kilikuwa kimeshafika Pwani ya nchi yetu lakini pia Pwani ya Msumbiji."Kimbunga hiki tayari kimekuwa na jicho, hivyo kina nguvu kubwa zaidi na jinsi kinavyoendelea kusogea kuelekea katika Pwani kinaendelea kuongezeka nguvu na kwa sasa kina mgandamizo wa 936 ambao ni mdogo.


"Mgandamizo huo unavuta upepo kuekelea kwenye kimbunga hicho na kasi ya upepo kwa sasa ni kilometa 130 kwa saa lakini kadri kinavyozidi na kasi inaongezeka na hivyo tunatarajia kuwa na kasi ya kilometa 140 kwa saa,"amesema Dk.Kijazi.

Amefafanua kesho Aprili 26, 2019 kimbunga Kenneth kitakuwa kinatuka nchi kavu nchini Msumbuji na kitakuwa na umbali wa kilometa 237 kutoka eneo la Pwani ya Mtwara. Kwa kawaida kimbunga kinapotua kinapunguza nguvu ya ule upepo lakini upepo huo lazima utasababisha athari katika maeneo ya nchi kavu.

"Kwa kasi ya upepo wa kimbunga hicho ambacho ni kikubwa kuwahi kutokea athari zake zinaweza kuikumba mikoa ya Lindi,Ruvuma na Mtwara yenyewe, hivyo ni vema wananchi wakachukua tahadhari kuepuka maafa ya watu na uharibifu wa mali na miundombinu na hasa kwa kuzingatia kitaongeza pia kna cha bahari.

Amefafanua kwa Mkoa wa Mtwara mvua ambazo zimeanza kunyesha wananchi wanaweza kuziona ni za kawaida lakini kadri kimbunga kinavyosogea ndivyo ambavyo mbunga kinavyoongezeka." Kimbunga kitakuwa katika nchi kavu hadi Jumatatu kabla ya kurudi tena baharini.Hivyo tuchukue tahadhari kwa kipindi chote hicho na TMA tutaendelea kutoa taarifa ya muelekeo wa kimbunga Kennethi,"amesema Dk.Kijazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...