Kumezuka hofu ya kimbunga kwenye upwa wa magharibi wa Bahari ya Hindi hususan katika nchi za Msumbiji na Tanzania.
Mtandao uliobobea kwenye masuala ya hali ya hewa wa AccuWeather wa nchini Marekani umeripoti kuwa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa katika bahari ya Hindi huenda ukapelekea kutokea Kimbunga kitakachopewa jina la Kenneth.
Iwapo kimbunga hicho kitatokea, kinatazamiwa kuathiri maeneo ya kuanzia Lindi kusini mwa Tanzania mpaka Pemba kaskazini mwa Msumbiji.
Mtandao huo pia umebainisha kuwa mgandamizo huo wa baharini unaweza kupoteza makali na kimbunga kisitokee, ila badala yake mvua kubwa zinaweza kutokea na kuathiri maeneo hayo.
"Mvua kali zinazoweza kusababisha mafuriko na mmomonyoko wa udongo katika maeneo kama Masasi na Tunduru nchini Tanzania, pia Marrupu na Montepuez kwa upande wa Msumbiji," imeeleza taarifa ta AccuWeather.
Kusoma zaidi Bofya Hapa>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...