Na Khadija Seif, Globu ya Jamii

KAMPUNI ya Said Salim bakhresa  imeingia makubaliano ya kibiashara na kampuni ya Nichol PLC kwa ajili ya uzalishaji wa kinywaji cha Vimto.

Mwakilishi kutoka kampuni ya Nichol PLC, Robert Hammersley amesema ni matumaini kuwa makubaliano hayo yataongeza pato la taifa kupitia uzalishaji wa kinywaji hicho cha Vimto.

Pia ameeleza kuwa ni wakati wa kuburudika na kinywaji hicho kutokana na kuzalishwa hapa nchini kwa sasa.

"Kinywaji cha Vimto kinaburudisha na hakina madhara na kinaweza kutumiwa kwa  rika lolote ," alisema  Hammersley.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kampuni ya Bakhresa, Said Salim    amesema makubaliano hayo ni fursa kubwa kwa nchi pamoja na kampuni ambayo imepata ikiwa ni ishara tosha kwa ubora wa bidhaa unazingatiwa kwa hali ya juu.

Aidha, kinywaji cha vimto kinatambulika ulimwenguni kote kinachopatikana katika vionjo kama vile soda ,juisi na peremende .

"Kwa sasa kinywaji cha Vimto kitazalishwa hapa nchini na kuuzwa kwa bei nafuu ili kuwafikia wanywajwi wote," 

Hata hivyo salim ametoa rai kwa wazalishaji wote wa bidhaa mbalimbali kuboresha bidhaa zao ili waweze kupata mikataba na masoko ya nje ya nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...