Chama cha Karate mtindo wa “Okinawa Goju Ryu” shina la Jundokan lenye
makao yake makuu Asato, mji wa Naha, kisiwa cha Okinawa, Japan, kwa mara
nyingine tena, kimetoa mwaliko kwa mwakilishi wa tawi la chama hicho nchini
Tanzania “Shibu-Cho Tanzania”, sensei Fundi Rumadha anaye shikilia ngazi ya
Dan 4 kushiriki kongamano litalofanyika mjini Vienna, Austria julai 18 hadi 21,
2019. Tokea uteuzi wake kama mkuu wa chama hicho Tanzania, sensei Fundi
ameweza kuwa pandisha ngazi wanafunzi wapatao 12 ngazi za Shodan na Nidan
hapa Tanzania.
Kutokana na maelezo ya wenyeji wa kongamano hilo mkuu wa chama cha
Jundokan Austria Dr. Friedrich Gsodam sensei mwenye kushikilia ngazi ya
“Hanshi”, Dan 9, ambaye alijifunza Karate chini ya mwanzilishi wa chama hicho
master Eiichi Miyazato tangu mwaka 1966, ameweza kukiri na kupendezwa na
juhudi za sensei Fundi kuwasaidia wana Jundokan wa Tanzania kufikia ngazi za
juu katika Sanaa hii ya Karate.
Viongozi wakuu wa chama hicho cha Jundokan na ujumbe wa Japan utaongozwa
na mwenyekiti wake Kancho Yoshihiro Miyazato na ujumbe wa masters au
magwiji wa Sanaa hiyo wakiwemo master Tetsu Gima Dan 9, na Sensei Yutaka
Oshiro toka Okinawa, Japan.
Tanzania, chini ya mkufunzi wake sensei Rumadha
na Angola chini ya mkufunzi sensei Filomeno ni wataungana na masensei toka
Afrika ya kusini, Madagascar, Israel, Argentina, Chile, na mataifa ya ulaya kama
Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Poland, Ureno, Corscica, Italy, Urusi, Lithuania,
Sweden, Azerbaijan, Scotland, Ireland na Hispania.
Waalikwa watawasili siku ya Alhamisi Julai 18, 2019 katika sehemu maalum ya
kijitongoji cha Hollabrunn Vocationa College pembezoni mwa jiji la Vienna,
Austria. Kongamano hilo la pekee bala la Ulaya, litafunguliwa kwa semina ya
masensei wa matawi yote kwa marekebisho na usahihi wa mbinu tofauti na
utumiaji mbinu za kujilinda ikiwemo kata za Sepai, Kururunfa, Sesan na
Suparinpei.
Siku ya pili itafuatiwa na mafunzo yatayogawanywa kwa ngazi za mkanda
mweupe hadi kahawia, kata za Gekisai dai ichi, Gekisai dai Ni, Saifa, Seiyunchin
na Shisochin, na Sanseiru mikanda mieusi Shodan ha Sandan ngazi ya tatu, na hali
kadharika nngazi ya nne hadi ya nane, Sanchin na Tensho kata. Nk.
Sensei Fundi anapenda kutoa shukrani zake kwa faraja ya kuwa mmoja ya walimu
hao mahili kuhudhuria hayo makongamano muhimu katika ulimwengu wa Karate.
Tayari sensei Fundi amesha pata fursa kubwa za kufanya mafunzi kama hayo na
masensei au masters wakuu wa Jundokan Karate huko Leeds, UK, Lisbon, Ureno,
Warsaw, Poland na hivi karibuni huko Okinawa, Japan. Pia vilevile, sensei Fundi
ataelekea Warsaw, Poland akifuatana na mkewe kwa mwaliko maalum toka mkuu
wa Jundokan Poland, sensei Monia Wysocka mwenye Dan 6.
“Lengo na tumaini la Jundokan Tanzania, ni kuwa na walimu wa ngazi za juu wa
Karate walio mahili katika sanaa na wanaotambulika chini ya baraza la chama
hicho huko Okinawa, Japan”, alisema sensei Fundi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...