Katika ulimwengu wa soka kuna mechi chache sana zinazoweza kuamsha hisia kama derby ya Der Klassiker ambayo itapigwa Jumamosi hii katika dimba la Allianza Arena, ngome ya Bayern Munich.

Mechi ya jumamosi ni zaidi ya derby ya kawaida kwa sababu timu zote mbili zinawania Ubingwa wa Bundesliga. Borussia Dortmund walirejea kileleni mwa ligi baada ya ushindi wa dakika za lala salama kwa mabao 2-0 dhidi ya Wolfsburg, huku Bayern wakidondosha alama mbili baada ya kutoka sare ya bao 1-1 ugenini kwa Freiburg.

Hivyo mchezo wa jumamosi utawafanya Bayern kupanda kileleni kwenye msimamo wa ligi endapo watashinda. Borussia Dortmund wao wanatakiwa kuepuka kufungwa ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kuchukua ubingwa wa Bundesliga. Dortmund watataka kujifunza kutoka kwa Liverpool wanaofundishwa na kocha wao wa zamani Jurgen Klopp ambaye aliwafunga Bayern wiki tatu zilizopita katika uwanja wao wa nyumbani Allianz Arena na kuwatoa katika hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa barani Ulaya. Kumbe Bayern wanaweza kufungwa nyumbani.

Ila Kocha wa Bayern anafahamu vizuri kuwa anahitaji ushindi dhidi ya Dortmund kwa gharama yoyote. Akiongea baada ya sare ya Freiburg alisema, “Nadhani wachezaji wanajua nini tunatakiwa kufanya. “Tunatakiwa kuwaonyesha Dortmund kwamba tunataka kuwa mabingwa naninatagemea tutacheza mchezo mzuri dhidi yao” Bayern wametangaza usajili wa wachezaji wapya kwa msimu ujao kama vile Kai Havertz wa Bayer Leverkusen. Usajili wa aina hii unaweza kusaidia kuongeza au kupunguza morali kwa baadhi ya wachezaji kama Jerome Boateng ambaye anaweza kuhisi hahitajiki tena kikosini hapo hivyo kuathiri kiwango chake uwanjani.

Wachezaji wa Dortmund wanaenda Allianz morali yao ikiwa juu baada ya ushindi wa dakika za majeruhi walioupata wikendi iliyopita dhidi ya Wolfsburg – Shukrani kwa magoli ya Paco Alcacer dakika ya 90 na 94. “Ni muhimu sana kushinda mchezo ujao jijini Munich na kila mtu anajua hilo” alisema kiungo wa Dortmund na timu ya taifa ya Ubelgiji Axel Witsel. “Hakuna mtu aliyetegemea Bayern watadondosha alama dhidi ya Freiburg na sasa tunaongoza ligi hatutakiwi kubadilika. Tutaenda Munich na morali hii na tutafanya kila tuwezalo ili tushinde”

Bayern Munich na Borussia Dortmund watakuwa wanakutana kwa mara ya mia moja Jumamosi hii na katika kuadhimisha uhasimu wao watabadilishana rangi za sare zao, Bayern wakivaa sare za njano huku Dortmund wakivaa sare nyekundu. Mchezo utaanza saa 1:30 Usiku na kuonyeshwa na kituo cha ST World Football kwenye king’amuzi cha StarTimes pekee. Watumiaji wanaweza pia kuchagua kuutazama mchezo na kupata uchambuzi kwa lugha ya Kiswahili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...