Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Dk.Binilith Mahenge amesema wananchi wa Mkoa wa Dodoma wanamshukuru Rais Dk.John Magufuli kwa uamuzi wake wa kuhamisha rasmi shughuli za makao makuu ya Serikali mkoani humo tena kwa vitendo.

Dk.Mahenge amesema baada ya Rais Magufuli kutangaza Serikali kuhamia Dodoma ,wananchi wameshuhudia zikitengwa fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo mikubwa inayofanyika kwa vitendo na wananchi wanaona utekelezaji unavyoendelea.

Akizungumza leo Aprili 13,2019 wakati wa uzinduzi wa Mji wa Serikali mkoani Dodoma ambapo Dk.Mahenge amesema Rais Magufuli ameandika historia kwa uamuzi wake wa kuamua shughuli za Serikali kuhamia Dodoma rasmi na kutekeleza maagizo yake kwa vitendo.

Amesema ujenzi wa soko kubwa la.kisasa,kituo kikubwa cha mabasi,hospitali,shule na miundombinu mingine inaendelea kutekelezwa na ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji wake na wananchi wamekuwa mashahidi kwa kazi nzuri ambayo inaendelea ndani ya Dodoma.

"Wananchi wa Dodoma wanashukuru kwani maamuzi yako Rais Dk.Maguful yamesababisha uchumi wa Dodona kukua kwa kasi kubwa na sasa wananchi wanafurahia uwepo wa Serikali.

"Baada ya kuanza kutekelezwa kwa ujenzi wa miradi ya maendeleo shughuli za ukuaji uchimi nazo zimeshika kasi hapa Dodoma.Tunakushukuru Rais kwa uamuzi wako," amesema Dk.Mahenge.

Amefafanua kuwa wakati leo zikizonduliwa ofisi za wizara na nyumba Serikali tayari jana na juzi baadhi ya mataifa yakiwamo ya China,Ujeruman Na Umoja wa Mataifa(UN)/wamefungua ofisi zao katika Mkoa huo wa Dodoma.

Ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa Watanzania kwenda kuwekeza Mkoa wa Dodoma kwani kuna kila kitu na maeneo ya uwekezaji yapo na yamepimwa,hivyo haoni sababu ya wawekezaji kuchelewa kwenda kuwekeza ndani ya mkoa huo.

Awali Waziri Mkuu mstaafu John Malecela amesema Rais Dk.Magufuli jina lake libaki katika mioyo ya wananchi wa wa Mkoa Dodoma na kwamba hivi sasa unaipotaja Dodoma unataja na Magufuli.

Uamuzi wako wa kuhamishia shughuli rasmi Dodoma ,Rais wetu unabaki kwenye mioyo ya wananchi wa Dodoma .Tutakumbuka kwa kizazi hiki na kizazi kijacho kadri dunia itakavyoendelea kuwepo,"amesema Malecelela.

Kwa kukumbusha tu Rais Magufuli Julai 25, 2016 alitoa tamko la kuhamishia Serikali Dodoma kutola Dar es Salaam kwa lengo la kusogeza huduma kwa wananchi wote na hatimaye leo hii Serikali imeshahamia Dodoma kwa kukamilika kwa Mji wa Serikali pamoja na ofisi ya Rais iliyoko Chamwino ambayo nayo imekamilika.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Dk.Binilith Mahenge

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...