Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

 Maambukizi ya Ukimwi kwa vijana yamezidi kuongezeka na kufanya serikali kushindwa kufikia malengo kutokana vijana ndio nguvu kazi ya taifa.

Hayo aliyasema Mkurugenzi wa Baraza la Uwezeshaji Kiuchumi Bengi Issa kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu wa Binge ,Vijana na Walemavu wakati Mkutano wa Wadau wanaotekeleza Afua za Wasichana Balehe na Wanawake Vijana Tanzania uliondaliwa na Tume ya Kudhibiti Ukimwa Nchini (TACAIDS) uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Issa amesema kuwa kutokana na hali hiyo vijana lazima muambiane ukweli kuhusiana na maambukizi ya Ukimwi kwa vijana wasichana walio katika balehe.Amesema serikali imekuwa ikitekeleza miradi ya Ukimwi ambapo aliongeza kuwa itaendelea kutoa ushirikiano kwa katika kufikia malengo ya kutomeza ugonjwa huo.

Issa amesema kuwa vijana katika kukabiliana na ugonjwa wa Ukimwi lazima teknolojia zilizopo zitumike katika kupeana habari.Bengi amesema mapambano ya ukimwi yafanyike kwa kila mtu katika nafasi yake kwani bila kufanya hivyo tutapoteza nguvu kazi ya taifa ambayo wahanga wakubwa ni wasichana walio katika Balehe na wanawake vijana.

Amesema afua hizo zimefanyika katika mikoa tisa lakini serikali itaendelea kushirikiana katika kumaliza mikoa yote.Nae Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi nchini (TACAIDS) Jumanne Isango amesema mkutano wa wadau wa muhimu katika kupeana mrejesho kwa utekelezaji wa mradi.

Amesema mapambano ya Ukimwi yanaendelea kwani bila kufanya hivyo nguvu kazi ya taifa itapungua na kushindwa kufikia katika ukuaji wa uchumi.Amesema vijana wasichana wanaoshiriki katika mradi wa sauti wameaswa kuendelea kuwa mabalozi ya kutoa elimu ya ukimwi katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kutumia teknolojia zilizopo katika karne ya 21.

Mwakilishi wa Unicef Urike Gilbert-Nandra amesema kuwa Unicef itaendelea kushirikiana na Tacaids katika mapambano ya ukimwi ili kuweza kufikia malengo.
 Mgeni Rasimi akiwa katika picha ya pamoja na wasichana walio katika mradi.
 Wadau katika mkutano wa TACAIDS
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Nchini (TACAIDS) Jumanne Isango akitoa maelezo ya uandaji wa mkutano wa Mwaka wa Wadau Wanaotekeleza Afua Wasichana Balehe na Wanawake Vijana Tanzania uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Wadau wa Mkutano Tacaids
 Mwakilishi wa Unicef. Urike Gilbert-Nandra akitoa maelezo namna Unicef inavyoshiriki katika mapambano ya Ukimwi katika mkutano wa mwaka wa Wadau wanaotekeleza afua za wasichana Balehe na wanawake vijana Tanzania uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Baraza la Uwezeshaji Kiuchumi Bengi Issa akizungumza katika Mkutano wa Mwaka wa Wadau wanaotekeleza Afua za Wasichana Balehe na Wanawake vijana Tanzania Uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...