Madaktari Bingwa wa MOI, Cuba pamoja na Bugando wakifanya upasuaji mkubwa wa kuondoa uvimbe kwenye ubongo

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dkt Philis Nyimbi akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) katika hafla ya kufunga kambi ya upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu iliyofanyika Bugando.


Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akieleza namna MOI ilivyojipanga kusogeza huduma kwa wananchi kwa kufanya kambi za uapasuaji, katika hafla ya kufunga kambi ya Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu iliyofanyika Bugando
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya rufaa ya Bugando Profesa Makubi akitoa taarifa ya namna kambi ya upasuaji iliyoendeshwa kwa ushirikiano kati ya MOI ,Bugando na Cuba 

 …………………….

Taasisi ya tiba ya Mifupa MOI,Cuba wameungana kwa pamoja na hospitali ya rufaa ya Bugando katika kambi ya upasuaji wa Ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu ambayo ilikuwa inafanyika mkoani Mwanza.

Zaidi ya wagonjwa 400 wamehudumiwa kati yao 17 wakifanyiwa upasuaji mkubwa na jopo la madaktari hao bingwa toka tarehe 8/04/2019 hadi 12/04/2019.

Akihitimisha kambi hiyo Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Dkt Philisi Nyimbi amemshukuru rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuri kwakufanya maboresho makubwa hapa nchini hususani kwenye huduma za afya.

“Kambi hii ya upasuaji wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu imeweza kutokana na maboresho yaliyofanya na serikali ya awamu ya tano, kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mwanza Ndg. John Mongela tunawashukuru wakurugenzi wakuu wa MOI na Bugando pamoja na madaktari bigwa wote, kwa hili wananchi wa kanda ya ziwa wamenufaika sana”. Amesema Dkt Philisi.

Mkurugenzi mtendaji wa MOI Dkt Respicios Boniface amesema hii ni sehemu ya mkakati wa MOI na serikali kuhakikisha huduma za kibingwa zinawafikia wananchi wote hususani wa mikoa ya pembezoni.

“Baada ya serikali kufanya uwekezaji mkubwa MOI, rufaa za nje ya nchi zimepungua sana hivi sasa wa MOI na serikali ni kuhakikisha huduma za kibigwa zinawafikia wananchi wote”. Amesema Dkt.Boniface.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa hospitali ya Bugando Profesa Abeli Makubi ameushukuru uongozi wa MOI kwa kukubali kuleta madaktari bingwa mkoani Mwanza ambao wamewahudumia wakazi wa kanda ya ziwa na kuwapunguzia adha ya kusafiri kwenda Dar es Salaam au nje ya nchi.

“Kwa niaba ya bodi pamoja na menejimenti ya hospitali ya Bugando tunawashukuru wenzetu wa MOI,Cuba kwa kuja kushirikiana nasi hapa kwenye kambi yah ii, tunaamini huu ni mwanzo wa ushirikiano baina ya taasisi zetu wakazi wa kanda ya ziwa wataendelea kunufaika”. Amesema Prof. Makubi..

Taasisi ya MOI imekuwa ikitekeleza kwa vitendo maagizo ya serikali ya kuhakikisha inawaongezea wananchi wa mikoa ya pembezoni huduma za kibigwa ili kuwapunguzia adha ya kusafiri kuzifuata huduma hizo MOI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...