Wadau wa Maendeleo mkoa wa Shinyanga wakiongozwa na Kampuni ya La Prince Pub inayojihusisha na biashara ya uuzaji vinywaji na chakula Mjini Shinyanga wamesherehekea Sikukuu ya Miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kutembelea na kuwapatia misaada mbalimbali wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Miongoni mwa zawadi zilizotolewa kwa akina mama na watoto ni pamoja na sabuni,mafuta ya kujipaka juisi,poda, miswaki,dawa za meno,matunda, toilet papers,biskuti,maji na zawadi zingine.

Wadau walioungana na wafanyakazi wa La Prince Pub kutembelea na kutoa misaada kwa wagonjwa leo Aprili 26,2019 ni pamoja na Kampuni ya Lulekia,Jambo Food Products Co. Ltd,Astro Secure Co. Ltd,Uptown Holdings Co.Ltd,Msirikale Microfinance,24 Security Tanzania,Ommy Fashion, Gvenwear,Shirika la TVMC,Dellah Car Traders,Luxury Pub,Friends of Bhoke na Malunde 1 blog.


Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo,Mkurugenzi wa Kampuni ya La Prince, Athanas William alisema wameamua kuungana na wadau wa maendeleo mkoa wa Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kurudisha fadhila kwa jamii inayowazunguka.

Alisema zawadi hizo kwa wagonjwa zimetolewa kupitia Mpango maalumu ulioanzishwa na La Prince Pub unaojulikana kwa jina la ‘La Prince Charity Movement’ kwa lengo la kuisaidia jamii kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo yakiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali,makampuni na wafanyabiashara mbalimbali. 

“Tumefika hapa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kutoa pole kwa wagonjwa na kuwapa misaada mbalimbali,tumejumuika sisi wafanyakazi wa La Prince na wadau wengine wa maendeleo wakiwemo kutoka kwenye mashirika na makampuni ambao tumeungana kuja kurudi kurudisha fadhila kwa jamii kwa kutoa misaada kwa wagonjwa katika wodi za akina mama na watoto",alisema.

“Tukiwa sehemu ya jamii tumeona ni busara zaidi katika siku hii ya kuadhimisha miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambayo hatufanyi sherehe za kitaifa,sisi tumeona tufanye sherehe ndogo ya kuwapa pole wanaoumwa na wenye mahitaji maalumu”,aliongeza William.

“Kilichotusukuma sisi ni moyo wa upendo,sisi tuna mpango maalumu unaitwa La Prince Movement ambapo kila mwezi tumeamua kuunganisha wadau mbalimbali wa mkoa wa Shinyanga kutoa misaada mbalimbali katika kada mbalimbali, leo tumeanza na hospitali na hivi karibuni tutambelea magereza”,alieleza Mkurugenzi wa La Prince Pub.
Mkurugenzi wa Kampuni ya La Prince, Athanas William akizungumza katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga wakati wadau mbalimbali wa maendeleo walipotembelea wagonjwa na kuwapatia zawadi akina mama na watoto waliolazwa katika hospitali hiyo leo Aprili 26,2019 ikiwa ni siku ya maadhimisho ya miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mmoja wa wafanyakazi wa La Prince Pub akiweka sawa zawadi mbalimbali zilizotolewa na wadau wa maendeleo mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya akina mama na watoto waliolazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Baadhi ya wafanyakazi wa La Prince Pub wakiwa wamebeba zawadi mbalimbali.
Wadau wa maendeleo wakiwa na zawadi zao wakijiandaa kuingia katika wodi mbalimbali katika hospitali ya rufaa mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kugawa zawadi hizo kwa wagonjwa.
Wadau wa maendeleo wakielekea katika wodi za watoto.
Mkurugenzi wa Kampuni ya La Prince, Athanas William akizungumza katika moja ya wodi akielezea lengo la wadau kufika katika hospitali hiyo.
Wadau wa maendeleo wakiwa wodini na zawadi zao kabla ya kuanza kuzigawa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya La Prince, Athanas William akisalimiana na mmoja wa Madaktari katika hospitali ya rufaa mkoa wa Shinyanga aliyekutwa wodini.
Wadau wakitoa zawadi kwa mama aliyelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi wa Kampuni ya La Prince, Athanas William akizungumza katika moja ya wodi za akina mama.
Wafanyakazi wa Ommy Fashion wakitoa zawadi kwa mgonjwa.
Wafanyakazi wa La Prince Pub wakitoa zawadi katika wodi ya watoto.
Mkurugenzi wa Kampuni ya La Prince, Athanas William akisalimia akina mama katika wodi ya watoto.
Utoaji zawadi ukiendelea katika wodi ya akina mama waliojifungua. katikati ni Bhoke Wambura, muanzilishi wa Friends of Bhoke.
Wadau wakiongozwa na Mkurugenzi wa shirika la TVMC,Musa Jonas Ngangala (katikati) wakikabidhi zawadi ya ndoo ya sabuni na zawadi zingine kwa mama aliyejifungua watoto mapacha wa kiume.
Wafanyakazi wa La Prince wakimsalimia na kumpa pole pamoja na zawadi mama wa mmoja mfanyakazi mwenzao aliyelazwa katika wodi ya wanawake.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...