Taasisi ya Young scientist Tanzania (YST) imeandaa maonesho ya wanasayansi chipukizi kwa mwaka 2019 yatakayofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere Internationa  Convention (Centre JNICC) Julai 31.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mwasisi YST Dkt. Gozbert Kamugisha amesema kuwa wanafunzi wa shule za Sekondari wanaendelea kufanyia kazi tafiti zao za kisayansi na Teknolojia chini ya ushauri wa taasisi hiyo wanaotembelea na kufanya nao tafiti mashuleni mwao.
Amesema wanafunzi wenye nia ya kushiriki maonesho hayo watume maombi na maelezo ya tafiti zao kwenda katika taasisi hiyo kabla ya Aprili 25.
Dkt Kamugisha amesema baada ya maombi hayo wanafunzi 200 wenye wenye tafiti za kiwango bora ndio watakuwa washiriki wa maonesho hayo.
Amesema YST 2019 pamoja na mpango wa kutembelea shule mbalimbali kuelekeza wanafunzi namna ya kufanya tafiti za kisayansi na ugunduzi wa teknolojia umedhaminiwa na Shell Exploration and Production Limited na Karimjee Jivanjee  Foundation (KJF)/ Toyota Tanzania.
Dkt Kamugisha amesema tafiti za kisayansi zitakazojumuishwa katika ya YST 2019 zitakuwa katika nyanja mbalimbali za kisayansi za Kemia ,Fizikia na Hesabu ,Biolojia na Mazingira, Sayansi ya Jamii na Teknolojia na hizo tafiti ni zile zinazojaribu kutafuta njia za kukabiliana na changamoto za Afya,Kilimo,Usalama wa Chakula ,Usalama wa Mawasiliano na Usafirishaji,Nishati ,Elimu pamoja na Mabadiliko ya Tabianchi.
Amesema wanasayansi Chipukizi wataofanya ugunduzi mzuri zaidi watazawadiwa fedha ,Medali Matengenezo ya maktaba ya shule pamoja na vitabu na mmoja wadhamini KJF pia itatoa zawadi udhamini wa masomo ya chuo kikuu kwa wanafunzi wenye ugunduzi wenye ubora wa kiwango cha juu ili kuwawezesha kusoma elimu ya chuo kikuu katika kusoma elimu ya chuo kikuu katika masomo ya kisayansi na teknolojia.
Hata hivyo amesema mpango wanasayansi YST kutembelea shule mbalimbali kuwafundisha wanafunzi namna ya kufanya utafiti na ugunduzi wa teknolojia pamoja na maonesho ya wanasayansi chipukizi ya kila mwaka vimesaidia kuwapa ujuzi muhimu wanafunzi katoka kutafuta njia za kumaliza changamoto za kijamii na kiuchumi kwa kutumia sayansi na kujenga utamaduni wa kisayansi kwa vijana.
Taasisi imewaomba wadau kujitokeza katika udhamini wa maonesho hayo.
 Mkurugenzi na  Mwanzilishi wa Tasisi ya Tanzania Young Scientist(YST), Dr. Gozbert Kamugisha  akizungumza jambo na waandishi  hawapo pichani wa habari juu ya Maonesho ya wanasayansi chipukizi kufanyika Julai 31 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Karimjee Foundation, Yusuf Karimjee akieleza waandishi wa habari namna gani tasisi yake ilivyoweza kudhamini wanafunzi 27 tangu mashindano na maonyesho ya Sayansi yaanze nchini.

mkutano ukiendelea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...