Mkurugenzi wa Sensa ya Takwimu za Kijamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya hali ya mfumuko wa bei wa kipindi cha Mwezi Machi mwaka huu.
…………………….
 
Na.Alex Sonna,Dodoma 


Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) imesema kuwa mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia Machi mwaka huu umeongezeka kidogo hadi asilimia 3.1 kutoka 3.0 sawa na ongezeko la asilimia 0.1.

Hayo yamesemwa leo jijini hapa na Mkurugenzi wa Sensa ya Takwimu za Kijamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo, wakati akitoa taarifa ya hali ya mfumuko wa bei wa kipindi hicho.

Bw.Kwesigabo ameeleza kuwa kuongezeka kwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioshia Machi mwaka huu kumechangiwa hasa na kuongezeka kwa bei za bidhaa zisizo za vyakula zikilinganishwa na bei za mwaka ulioishia Machi mwaka jana.

“Hiyo inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Machi mwaka huu imeongezeka kidogo ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia Februari,” amesema Kwesigabo

Aidha amefafanua kuwa kuongezeka kwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioshia Machi mwaka huu kumechangiwa hasa na kuongezeka kwa bei za bidhaa zisizo za vyakula zikilinganishwa na bei za mwaka ulioishia Machi mwaka jana.

Kwisegabo alitaja baadhi ya bidhaa hizo kuwa ni pamoja na mavazi na viatu(4.4%), kodi ya pango(4.7%), mafuta ya taa(1.8%), dizeli(8.3%), chakula na vinywaji kwenye migahawa(4.6%) na malazi kwenye mahoteli(5.7).

Hata hivyo amefafanua kuwa mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa machi mwaka huu umepungua hadi asilimia 0.1 kutoka asilimia 0.5 kwa mwaka ulioishia Februari mwaka huu. Kuhusu hali ya mfumko wa bei kwa nchi za Afrika Mashariki alisema nchini Uganda kwa mwezi ulioishia Februari mwaka huu umebaki asilimia 3.0 kama ilivyokuwa ulioishia Februari.

Pia Kwesigabo ameongeza kuwa kwa upande wa Kenya mfumuko kwa mwaka ulioishia Machi mwaka huu umeongezeka hadi asilimia 4.35 kutoka 4.14 kwa mwaka ulioishia Februari mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...