Mariam Rajab (25), mkazi wa Singida ambaye video yake imesambaa kwenye mitandao ya kijamii akiomba msaada wa matibabu, amewasili saa 6:00 usiku wa kuamkia leo  katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) yarai kuanza matibabu kwa udhamini wa serikali.

Mariam alipokelewa katika Idara ya Magonjwa ya Dharura ambapo amefanyiwa vipimo vya awali na kisha na kupelekwa kulazwa wodini ili aweze kuonana na jopo la madaktari bingwa wa upasuaji kwa ajili ya kupatiwa matatibu Zaidi siku ya Alhamisi.

“Mimi naitwa Mariam Rajabu naishi katika Mkoa wa Singida, Mtaa wa Mnung’una naishi katika familia ya kimasikini, wazazi wangu hawana uwezo wa kunisaidia tatizo langu, tatizo ambalo ninalo, tatizo lenyewe ambalo ninalo ni kidonda ambacho kipo hapa mgongoni, naombeni Watanzania wenzangu muweze kunisaidia niweze kwenda Hospitali ya Muhimbili ili niweze kupata matibabu. Sina cha kuwalipa bali Mungu atawalipa, asanteni” hayo ni maelezo aliyotoa Mariam kupitia picha ya video iliyoanza kusambaa katika mitandao ya kijamii mwanzoni mwa wiki hii na kuvuta hisia za watu wengi.
Kutokana na taarifa hiyo, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (MB) aliuagiza Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kumtafuta Mariam ili apelekwe Hospitalini hapa kwa ajili uchunguzi na matibabu.
Mariam ameletwa na gari la wagonjwa (ambulance) kutoka Singida lililoanza safari yake saa 8:00 mchana jana. Tutaendelea kuwapa taarifa juu ya mwenendo wa matibabu yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...