Na Ripota Wetu, Globu ya jamii

MTENDAJI Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Profesa Dos Sanatos Silayo amewataka waajiriwa wapya na wazamani wa wakala huo kuhakikisha wanatakeleza majukumu yao kadri sheria za nchi na jinsi maadili yanavyowataka.

Profesa Silayo ameyasema hayo leo Machi 3,2019 ambapo ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa anawapongeza watumishi hao kupata fursa ya kufanya kazi TFS lakini ni vema wakatambua wanalo jukumu la kutekeleza majukumu yao kwa kufuata misingi ya sheria za nchi. “ Niwapongeze watumishi wapya kwa kupata nafasi ya kufanya kazi nasi, lakini nataka kuwasisitizia suala la uadilifu na maadili katika utumishi si la mzaha, enendeni mkalitumikie taifa na kamwe msisubiri kufanya kazi kwa kusukumwa."

Ameongeza kuwa kila mmoja anatakiwa kufanya kazi kwa hiari, kwa kufuata sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyopo ili kuhakikisha utumishi wa umma unaleta tija iliyokusudiwa, hivyo amefafanua ndio maana wameamua pia watumishi wa zamani kuwapatia amafunzo haya ikiwa ni jitiada za kurejesha uadilifu na maadili miongoni mwao.

Kwa upande wake Mkuu wa Mafunzo ya muda mfupi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Charles Magaya aliyemwakilisha Kaimu Mtendaji Mkuu wa chuo hicho, Dk.Emanuel Shindika ameipongeza TFS kwa kutambua kuwa ili utumishi wa umma uwe wenye ufanisi na wa kuheshimika, watumishi wanapaswa kuzifuata Kanuni za maadili ya utumishi pamoja na kuwa na tabia na mwenendo unaozingatia utoaji wa huduma bora, utiii kwa Serikali, kutoa huduma bila upendeleo, kufanya kazi kwa uadilifu, kuwajibika kwa umma, kuheshimu sheria na matumizi sahihi ya taarifa kwa kuwapa nafasi yakuwafunza watumishi hao.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Profesa  Dos Sanatos Silayo akifafanua jambo wakati anazungumza na waajiriwa wapya na wa zamani wa wakala huo ambapo amewakumbusha kutekeleza majukumu yao kwa kuheshimu sheria za nchi na jinsi maadili ya umma yanavyoelekeza.
 Mkuu wa Mafunzo ya muda mfupi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Charles Magaya aliyemwakilisha Kaimu Mtendaji Mkuu wa chuo hicho, Dk. Emanuel Shindika akifafanua jambo ambapo pia ametoa pongezi kwa  TFS.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Profesa Dos Santos Silayo (aliyekaa mstari wa mbele katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wapya na wazamani wa wakala huo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...