Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.

OFISA wa Jeshi la Polisi nchini, Mrakibu Lydia Ngua (43) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashitaka 22 ya kujipatia fedha Sh. 489, 615,000 za upatu kutoka kwa watu mbalimbali wakiwamo maofisa wa jeshi hilo.

Akisoma mashitaka, Wakili wa Serikali, Ester Martin amedai mbele ya Hakimu Mkazi Augustina Mbando kuwa, jijini Dar es Salaam,  mshitakiwa  alijipatia Sh milioni 15.3 kutoka kwa Happy Mhando kwa nia ya kwenda kuziwekeza fedha hizo kwenye vikoba huku akijua kuwa anaenda kuzitumia kwa matumizi yake binafsi .

Imndai kuwa, Septemba 13, mwaka jana jijini Dar es Salaam, mshtakiwa Ngua alijipatia Sh milioni 13.2 kutoka kwa Elisia Kisoma. Pia katika tarehe na mahali kusikofahamika, jijini Dar es Salaam, mshitakiwa huyo alijipatia  Sh milioni 7.8.

Katika mashitaka mengine mshtakiwa Ngua alijipatia Sh  milioni 12.3 kutoka kwa Mariam Yohana.  zingine ni sh. Sh milioni 3.4 kutoka kwa Jenifa Fokanya. Sh. milioni 15 kutoka kwa Jane Martin, pia alijipatia Sh milioni 20.8 kutoka kwa WP Mary.

Fedha zingine alijipatia Shilingi milioni 10.9 kutoka kwa maofisa wa jeshi hilo ambao ni ASP, Imelda Twelve, Sh 9.040.000 kutoka kwa ASP Sarah Komba, Sh milioni 67 kutoka kwa Inspekta wa polisi, Richard Ninja na Sh milioni 27 kutoka kwa Shukuru Makaranga, Sh 115,897,000 kutoka kwa Henry Lwiza na Sh milioni 75 kutoka kwa Edna Mbeto

Ofisa huyo pia anadaiwa kujipatia Sh milioni 11 kutoka kwa Sabrina Mwakitalu, Sh milioni 23.3 kutoka kwa Lusiana Mwakitalu,  Sh.milioni sita kutoka kwa Mwanahamisi Issa, Sh milioni 3.78 kutoka kwa Mkemimi Abdulkarim, Sh milioni 191.4 kutoka kwa Zidadu Hassan,  sh milioni  4.322 kutoka kwa Innocent Nunuo, Sh milioni nane kutoka kwa WP Happy, na Sh milioni 37.7 kutoka kwa Halima Nabalanganya.

Imedaiwa kuwa mshitakiwa alijipatia fedha hizo kwa nia ya kwenda kuziwekeza kwenye vikoba huku akijua kuwa anaenda kuzitumia kwa matumizi yake binafsi.

Hata hivo, mshitakiwa amekana hayo na amerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza msharti ya dhamana ambapo mahakama imemtaka mshitakiwa kuwasilisha mahakamani hapo nusu ya fedha anazodaiwa au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.

Pia ametakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaotoka kwenye taasisi zinazotambulika na wawe na vitambulisho na wadhamini hao pia wametakiwa kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika ye kiasi hicho cha pesa. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 24, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...